Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameagiza kuundwa Tume ya uchunguzi vitendo vya ubakaji na mimba kwa wanafunzi katika Wilaya nzima ya Songea. Kanali Thomas ametoa maagizo hayo kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile baada ya kusikiliza kero za wananchi wa Kata ya Wino kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lilondo ambapo wananchi walidai kukithiri kwa vitendo vya ubakaji kwa wanawake na idadi kubwa ya wanafunzi kupata mimba na kuacha masomo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.