Mradi wa ujenzi wa njia za watembea kwa miguu zenye urefu wa mita 600 katika Hospitali ya Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma umekamilika kwa asilimia 100.
Mradi huu umegharimu Shilingi milioni 300 na tayari njia hizo zimeanza kutumika na wagonjwa wanaofika kupata huduma hospitalini hapo.
Fedha za utekelezaji wa mradi huo zilitolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ujenzi wa njia hizo unalenga kuwezesha wagonjwa na watoa huduma kutembea kwa urahisi na usalama, hivyo kupunguza usumbufu na hatari ya ajali katika maeneo ya hospitali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Sajidu Idrisa Mohamed, ameongoza timu ya wataalamu waliotembelea eneo la mradi huo na kutoa pongezi kwa wasimamizi wa ujenzi kwa kufanikisha mradi kwa ubora na kwa wakati.
Mradi huu umeibua matumaini mapya kwa wakazi wa Madaba na maeneo jirani, kwani utaboresha mazingira ya utoaji huduma za afya na kuongeza ufanisi katika kazi za watumishi wa hospitali hiyo.
Rais Samia ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya, hospitali na miundombinu mingine rafiki, ili kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa wananchi wote nchini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.