Viongozi wa serikali za vijiji 7 wakiwemo wenyeviti wa vijiji ,watendaji wa vijiji ,wenyeviti wa kamati ya maliasili wa vijiji na waheshimiwa madiwani kutoka katika kata za vijiji hivyo wamepatiwa mafunzo ya utawala bora kutoka FORVAC na MJUMITA.
Akifungua mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume Kizigo aliishukuru FORVAC na MJUMITA kwa jitihada zao za kutoa elimu kwa jamii kuhusu faida ya kutunza misitu yao iliyopo katika vijiji .
Kizigo alisema mafunzo hayo yapate wataalamu wa uhifadhi katika vijiji watakaosimamia utawala bora ili lengo la uhifadhi kwa jamii liongeze faida za kiuchumi,kijamii na kimazingira kutokana na usimamizi endelevu wa misitu yao.
Hata hivyo kizigo aliwataka viongozi wanaopata mafunzo hayo kuzingatia misingi ya utawala bora ya uwajibikaji,uwazi ,utawala wa sheria,maridhiano ,mwitiko,ushirikishwaji na kuleta ufanisi na tija katika jamii wanayoiongoza.
Maulidi Hamisi afisa misitu wilayani Namtumbo aliwaambia viongozi wa vijiji kuwa viongozi wa vijiji wengi wanaohudhuria mafunzo ya misitu hawatoi mrejesho kwa wananchi na badala yake hubaki nayo wenyewe hali inayosababisha wananchi kutoelewa dhana dhima ya uhifadhi wa misitu yao ya vijiji.
Hamisi aliwataka viongozi hao kwenda kutoa mrejesho kwa wananchi katika vijiji vyao ili wananchi waweze kujua maana na umuhimu wa uhifadhi wa misitu yao ya vijiji na kupunguza migogoro ambayo inasababishwa na kutotolewa taarifa kwenye mikutano ya maamuzi ya vijiji..
Naye Mwenyekiti wa mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu Tanzania bwana Revocatus Njau aliwataka viongozi hao wa vijiji kuwa mfano wa kusimamia utawala bora katika uhifadhi wa misitu katika vijiji vyao .
Diwani wa kata ya Mkongo Daniel Nyambo pamoja na kushukuru FORVAC na MJUMITA kwa mafunzo ya utawala bora alieleza tatizo la uhifadhi katika vijiji vya Namtumbo kuwa vijiji vinaweza kutenga maeneo ya hifadhi lakini wafugaji wameenea katika maeneo yaliyotengwa na kuharibu maana ya uhifadhi .
Alisema wakulima ni rahisi kuwaondoa lakini wafugaji inahitajika nguvu za ziada za dola kuhakikisha wafugaji wanaheshimu mipango ya vijiji wanajifugia mifugo katika maeneo ambayo hayastahili kupelekwa mifugo hiyo.
Mafunzo hayo yalikuwa ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wlaya ya Namtumbo na viongozi wa kijiji cha Kumbara,Limamu,kilangalanga,Chengena,Masuguru ,Njalamatata,Ligunga pamoja na madiwani wa kata ya luchili,mchomoro,mkongo,mkongo gulioni na limamu walihudhuria mafunzo hayo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.