• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

VITUO vya afya kumi vyajengwa Ruvuma kupitia tozo za miamala ya simu

Imewekwa kuanzia tarehe: September 16th, 2022

MKOA WA RUVUMA UNAVYOTEKELEZA MIRADI YA ZAIDI  BILIONI TANO KUPITIA TOZO YA MIAMALA YA SIMU

MKOA wa Ruvuma unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali  ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.362 katika Halmashauri zote nane kupitia tozo ya miamala ya simu.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema kati ya fedha hizo shilingi bilioni tano zimejenga vituo vya afya kumi  na zaidi ya shilingi milioni 360 zimejenga vyumba vya madarasa 29.

Amesema miradi hiyo inatekelezwa katika Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga miradi inayotekelezwa ina thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja.

Ameitaja miradi inayotekelezwa katika Halmashauri Mbinga kuwa ni  ujenzi wa kituo cha afya Mkumbi na kituo cha afya Kindimbachini vinavyogharimu shilingi bilioni moja na umaliziaji wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari Nyoni na  Litumbandyosi unaogharimu shilingi milioni 50.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa,Katika Halmashauri ya Madaba serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 525 kutekeleza miradi ya Kituo cha Afya Matetereka ambacho kinagharimu shilingi milioni 500 na  ujenzi wa madarasa mawili katika sekondari ya Lipupuma ambayo yanagharimu shilingi milioni 25.

RC Thomas ameitaja miradi inayotekelezwa kupitia  tozo ya miamala ya simu katika Halmashauri ya Mbinga Mji inagharimu  shilingi milioni 537 ambazo zinatumika kutekeleza miradi ya ujenzi wa kituo cha Afya Mbangamao ambacho kinatumia shilingi milioni 500 na  umaliziaji wa vyumba viwili vya madarasa katika sekondari ya Kilimani na chumba kimoja sekondari ya Lamata ambavyo vinagharimu zaidi ya shilingi milioni 37.

Kanali Thmoas amesema katika Halmashauri ya Namtumbo serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 537 ambazo zinatumika  kujenga kituo cha Afya Ligera ambacho kimetengewa shilingi milioni 500  na ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa sekondari ya Nasuli na vyumba viwili sekondari ya Mbunga ambavyo vinatumia zaidi ya shilingi milioni 37.

Kulingana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa inagharimu  shilingi milioni 537 ambapo shilingi milioni 500 zinatumika kujenga jengo la upasuaji,wodi ya akinamama katika kituo cha afya Liparamba,ujenzi wa nyumba ya watumishi wa afya,jengo la mionzi na njia ya kutembea wagonjwa.

Ameitaja miradi mingine inayotekelezwa katika Halmashauri ya Nyasa kuwa ni umaliziaji wa vyumba vya madarasa vitatu katika shule za sekondari Luhangarasi na Kingerikiti.

 Mkuu wa Mkoa ameitaja miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea kuwa ina thamani ya shilingi bilioni moja ambapo miradi inayotekelezwa ni ujenzi wa Kituo cha Afya Kilagano na kituo cha afya  Liganga kila kimoja kikiwa na thamani ya shilingi milioni 500.

Katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea  ameitaja miradi inayotekelezwa kupitia tozo ya miamala ya simu kuwa  ina thamani ya shilingi milioni 550.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni Kituo cha Afya Subira kinachogharimu shilingi milioni 500 na ukamilishaji wa vyumba  vinne vya madarasa katika shule za sekondari Lizabon,Luwawasi na Lukala vyenye thamani ya  zaidi ya shilingi milioni 37.

 Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,miradi inayotekelezwa kupitia tozo ya miamala ya simu katika Halmashauri ya Tunduru inagharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.

Hata hivyo amesema kati ya fedha hizo shilingi milioni 500 zinatekeleza ujenzi wa kituo cha afya Masonya na shilingi milioni 500 zinatekeleza mradi wa kituo cha afya Mchesi.

Miradi mingine inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo ni  ukamilishaji wa maboma katika shule za sekondari Masonya na  Mbesa kwa gharama ya shilingi milioni  25.

Imeandikwa na Albano Midelo,Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  Ruvuma

Septemba 16,2022

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.