Serikali imetoa shilingi milioni 161 katika shule ya msingi Lumeme Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya awali ya mfano,nyumba moja ya mwalimu ya familia mbili na matundu sita ya vyoo .
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Mohamed Ally imekagua mradi huo na kupongeza Usimamizi wa mradi uliosabibisha ubora wa mradi.
“sisi kama CCM tunaomba waandisi wengine nchini kote wafike Wilaya ya Nyasa kuona darasa la awali la mfano Tanzania “,alisisitiza Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma.
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma imemaliza ziara ya siku nane ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.