Maafisa Elimu Msingi kutoka Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wametembelea Shule sita za Msingi ambazo ni;- Mdwema, Utwango, Libobi, Suluti, Kanjele, na Nambalama zilizopo katika Wilaya ya Namtumbo ili kujua hali ya Wanafunzi katika Masomo na mwenendo wa walimu katika Ufundishaji.
Mwalimu Rhoda Mbilinyi ni Afisa Elimu Taaluma Msingi Wilaya ya Namtumbo ametoa wito kwa Walimu kuongeza jitihada kwenye ufundishaji makini wa Mada pia kusaidia wanafunzi katika kutatua changamoto zao na kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma na kuandika ili kuinua taaluma na elimu bora Katika Wilaya ya Namtumbo na Taifa kwa Ujumla.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.