Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameitaja moja ya changamoto kubwa katika shule za sekondari mkoani humo ni kuwepo kwa idadi kubwa ya walimu wanaume wanaofanya mapenzi na wanafunzi .
Kanali Thomas amesema hayo wakati anazungumza na wakuu wa shule za sekondari mkoani Ruvuma kwenye kikao cha tathmini ya elimu baada ya Mkoa kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa ambapo Mkoa umeshindwa kufikia lengo la ufaulu lililowekwa kitaifa la asilimia 100 kwa mtihani wa upimaji wa kidato cha pili.Ufaulu wa kidato cha pili mkoani Ruvuma mwaka 2023 ni asilimia 81.96
Akizungumza na wakuu wa shuke za sekondari Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwenye ukumbi wa Songea Gilrs amesisitiza kuwa baadhi ya walimu wanaume wanaofanya ngono na wanafunzi wanafahamika lakini wamekuwa wanabebwa na wakuu wa shule hivyo ametoa rai walimu wenye tabia za kwenda kinyume na maadili ya kazi ni vema wafichuliwe na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuwa walimu ni walezi hivyo kufanya mapenzi na wanafunzi ni kosa la kinidhamu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.