Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetoa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma PEPMIS na PIPMIS kwa watumishi wa Umma wa Halmashauri na Taasisi za Serikali ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Mafunzo haya yamefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Kilosa mjini Mbambabay.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watumishi wa Umma ili waweze kutoa Taarifa ya utekelezaji na kupimwa majukumu yao kupitia mfumo wa usimamizi wa utendaji kazi wa Utumishi wa Umma.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Idara na Sera na Mipango (ORMUUB) Bw Cyrus Kapinga amesema mafunzo haya ni muhimu kwa watumishi wa Umma kwa kuwa watakuwa wanatoa taarifa ya utendaji kazi na kupimwa kwa njia ya mfumo.
Amesema mafunzo hayo yatamwezesha mtumishi akiwa kwenye kituo chake cha kazi kutumia mfumo na mtumishi kuomba mikopo, uhamisho na shughuli nyingine nyingi.
Amesema Ofisi ya Utumishi imeamua kufika mikoani kwa ajili ya kufundisha na kufanya tathimini ya mfumo huu ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wanapotumia mifumo huo.
Ametoa rai kwa Watumishi kujifunza na kutumia mfumo huu kwa kuwa mfumo wa awali wa OPRAS ambao ulikuwa unapima utendaji kazi wa mtumishi wa umma umefutwa.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi kufungua mafunzo Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa Bw, Salum Ismail amewataka watumishi kufanya kazi kwa juhudi na kutoa taarifa ya utendaji kazi kupitia mfumo huu.
Watumishi waliopata mafunzo ni Wakuu wa Divisheni na Vitengo na watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa pamoja
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.