Na James Francis,Songea
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe, amezindua rasmi sheria na kanuni za urutubishaji wa chakula za mwaka 2024 katika ukumbi wa Chandamali, Manispaa ya Songea,.
Hii ni hatua muhimu katika kuimarisha afya ya Watanzania kwa kupambana na magonjwa yanayotokana na upungufu wa virutubisho.
Katika uzinduzi huo, Mhe. Kigahe alisisitiza kuwa sheria na kanuni hizo zinalenga kuhakikisha chakula kinakuwa na virutubisho muhimu kama njia ya kudhibiti matatizo ya lishe, hasa utapiamlo, udumavu, na upungufu wa vitamini.
“Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan alisaini mkataba wa lishe mwaka 2022 na kutoa maelekezo kwa Wizara yetu kuandaa kanuni hizi ili kukabiliana na changamoto za lishe duni,” alisema Kigahe.
Aliongeza kuwa sheria hizi zitaanza kutekelezwa rasmi miezi saba kuanzia Desemba, na mamlaka ya kusimamia ubora (TBS) itaanza ukaguzi wa wazalishaji wa vyakula husika.
Vyakula vinavyolengwa katika mpango huu wa urutubishaji ni pamoja na unga wa mahindi, unga wa ngano, mafuta na chumvi, ambavyo vitatakiwa kuongezewa virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu.
Mhe. Kigahe aliwasihi wadau kutoka sekta mbalimbali kushirikiana katika utekelezaji wa sheria hizi na kuwataka wazalishaji kujiandaa mapema kwa mabadiliko hayo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.