TAARIFA YA KIKAO CHA BARAZA LA USHAURI MKOA WA RUVUMA(RCC) DESEMBA 2022.doc
6.3.1.1 Huduma za Afya
Mkoa una jumla ya vituo 356 vinavyotoa huduma za afya. Kati ya vituo hivyo Hospitali ni 13 zikiwemo 6 za serikali, vituo vya afya 36 kati ya hivyo 10 ni vya mashirika ya dini, zahanati zipo 307 ambapo za serikali ni 246, Mashirika ya dini ni 26, na 9 ni za mashirika ya umma na 26 ni za watu binafsi.
Mapokezi ya Fedha za Utekelezaji wa Miradi ya maendeleo
Kwa mwaka 2020/2021 Mkoa umepokea jumla ya Shilingi 1,700,00.000.00 kwa ajili ya kujenga/kukarabati vituo vya kutolea huduma za afya ambapo Sh. 1,200,000,000.00 zilikuwa kwa ajili ya umaliziaji wa maboma 50 ya zahanati na Sh. 500,000,000.00 kwa ya kituo cha Afya Magazini.
Kwa mwaka 2021/2022 Mkoa umeendelea na ujenzi wa Hospitali tano (5) za Wilaya katika Halmashauri za Wilaya za Nyasa, Namtumbo, Madaba, Songea DC na Mbinga DC kwa gharama ya Tshs. 3,700,000,000.00. Mkoa umepokea kiasi cha Tshs. 7,250,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya 12 kupitia fedha za Tozo na Serikali Kuu. Pia Mkoa unaendelea na ujenzi wa vituo vya Afya vitatu (3) kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri kwa gharama ya Tshs. 1,500,000,000.00. Kwa upande wa Zahanati Mkoa ulipokea kiasi cha Tshs. 1,050,000,000.00 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa Zahanati 21 kwenye Halmashauri saba (7).
Aidha, Mkoa umepokea pia kiasi cha shilingi 1,780,000,000.00 za kutekeleza Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 - (Mradi Na. 5144 TCRP) kama ifuatavyo:
Shilingi Milioni 630,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Watumishi wa sekta ya Afya kwa Halmashauri 7 (Madaba DC, Songea DC, Mbinga DC, Nyasa DC, Mbinga TC, Namtumbo DC & Tunduru DC)
Shilingi Milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya dharura (emergency Medical Department-EMD) kwa Halmashauri za Madaba DC, Nyasa DC & Tunduru DC
Shilingi 250,000,000.00 kwa ajili ya Ujenzi wa jengo la huduma za Wagonjwa mahututi (ICU) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Taarifa ya Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
Mkoa ulipokea kiasi cha Tshs. 2,700,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa awamu ya kwanza ambao unahusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la mionzi na nyumba ya mtumishi.
6.3.1.2 Hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya
Hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya imeendelea kuimarika, kwani upatikanaji umeongezeka kutoka 93 (2021) hadi asilimia 96 mwezi Novemba, 2022. Upatikanaji huu umetokana na kuongezeka kwa mapato ya ukusanyaji ya mapato ya uchangiaji wa huduma za afya, ufuatiliaji na usimamizi pamoja na ruzuku ya dawa kutoka serikali kuu.
6.3.1.3 Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto
Vituo vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi na mtoto vimeongezeka kutoka 324 hadi 348 sawa na asilimia (98%) ya vituo vyote vinavyotoa huduma katika Mkoa. Kati ya vituo vinavyotoa huduma ya afya ya uzazi na mtoto, Vituo 316 sawa na asilimia 92 vinatoa huduma ya chanjo. Aidha kati ya vituo vya afya 36, vituo 14 (38.8%) ya vituo vya Afya (H/C) vinatoa huduma kabambe za dharura za mama wajawazito na Watoto wachanga (CEmONC).
Kwa upande wa huduma ya wazazi, kiwango cha akina mama waliojifungulia kituoni kimeongezeka kutoka asilimia 84.4 mwaka 2020 hadi asilimia 85.4 Desemba 2021. Kiwango hiki ni juu ya lengo la taifa la asilimia 80.
Jedwali Na. 47: Kuonesha mwenendo wa vifo vya kina mama wazazi Mkoa wa Ruvuma kwa miaka minne (4)- 2019-2022
Na
|
Mwaka
|
Idadi ya vifo
|
02
|
2019 |
34 |
03
|
2020 |
31 |
04
|
2021 |
24 |
05
|
2022 |
20 |
Idadi ya vifo vya wazazi vimepungua kutoka vifo 24 Disemba mwaka 2021 hadi vifo 20 sawa na vifo 39 /100,000 vizazi hai Novemba mwaka 2022. Sababu zilizochangia vifo ni Kutokwa na damu nyingi PPH, Kifafa cha mimba, mgando katika mishipa ya damu (Embolism), Upungufu wa damu na madhara ya dawa za usingizi (anaethetic complication).
Vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja kwa mwaka 2022 vimepungua kutoka 131 sawa na vifo 3 kati ya watoto 1000 waliozaliwa hai mwaka 2021 hadi vifo 88 sawa na vifo 2 kati ya watoto 1000 waliozaliwa hai Disemaba mwaka 2022. Sababu zilizochangia vifo hivyo ni magonjwa ya watoto wachanga (perinatal condition). Vifo 35 sawa na asilimia 40.0 Prematurity vifo 25 sawa na asilimia 28.4, Pneumonia vifo 13 sawa na asilimia15.0, Malaria vifo 7 sawa na asilimia 8.0, Septicemia vifo 5 sawa na asilimia 6.0 na Anaemia vifo 3 sawa na asilimia 3.4 ya vifo vyote.
Takwimu za vifo vya watoto chini ya miaka mitano vilivyotolewa taarifa ngazi ya vituo na jamii kwa mwaka 2022 vilikuwa 124 sawa na vifo 3 kati ya watoto 1000 waliozaliwa hai. Idadi ya vifo hivi imepungua ukilinganisha na vifo 204 sawa na vifo 4 kati ya watoto 1000 waliozaliwa hai mwaka 2021. Sababu zinazoongoza kwa vifo hivyo ni Neonatal condition vifo 41 sawa na asilimia 33.0, Pneumonia vifo 33 sawa na asiimia 26.6 malaria vifo 24 sawa na asilimia 19.3, Septicaemia vifo 15 sawa na asilimia 12.0 na Anaemia vifo 11 sawa na asilimia 9.0 ya vifo vyote.
6.3.1.4 Hali ya chanjo
Katika kipindi cha Januari hadi Novemba, 2022 Mkoa umekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za chanjo mbalimbali kama ifuatavyo;
Chanjo ya kifua kikuu (BCG) ni 141%, chanjo ya kuzuia kupooza (Polio) 125%, chanjo ya Donda koo, kukakamaa na kifaduro (DTP3) 123% chanjo ya kuzuia homa ya mapafu (Pneumonia) 122%, chanjo ya kuzuia kuharisha (Rota virus) 99.5%, chanjo ya surua (Measles Rubella) 122%, chanjo ya Pepopunda (Td) kwa wajawazito 117% na chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 ni 115%.
Mkoa umeendelea kutoa chanjo ya ugonjwa wa Korona ikiwa ni jitihada za kupambana na ugonjwa huu ambapo kwa kipindi cha kuanzia tarehe 04 Agosti, 2021 hadi tarehe 31 Oktoba, 2022 jumla ya watu 1,045,390 wamekamilisha dozi ya chanjo ya korona sawa na asilimia 109. Mkoa uliwekewa kuchanja jumla ya watu 670,577 ambao ni sawa na asilimia 70 ya watu wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea (ambao ni 957,938).
Mkoa wa Ruvuma umeongoza Kitaifa kwa utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupewa vyeti 2 na tuzo kwa vipindi tofauti tofauti kwa mwaka 2021 hadi Mei, 2022. Pia katika mazoezi ya Kitaifa ya utoaji wa chanjo ya polio Mkoa wa Ruvuma umefanya vizuri katika awamu zote 4 (awamu ya kwanza nay a pili Tuliongoza Kitaifa iliyofanyika mwezi Machi na Mei, 2022). Utoaji wa chanjo za kawaida tunaendelea kufanya vizuri tangu tutangazwe kuwa vinara 2021.
6.3.1.5 Huduma za VVU na UKIMWI
Kati ya vituo 356, vituo 328 sawa na asilimia 92 vinatoa huduma za unasihi na upimaji wa VVU (HTS); vituo 285 sawa na asilimia 80 vinatoa huduma za Kuzuia Maambuzi ya VVU toka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (PMTCT); vituo 147 sawa na asilimia 41 vinatoa huduma za tiba na matunzo ya VVU na UKIMWI (CTC); vituo 41 sawa na asilimia 12 vinatoa huduma za Dawa Kinga ya Kuzuia Maambukizi ya VVU (PrEP) na vituo 45 sawa na asilimia 13 vinatoa huduma ya Tohara ya Kitabibu kwa Vijana Wanaume (VMMC).
Kiwango cha maambukizi ya VVU katika Mkoa wa Ruvuma kimepungua kwa 1.4 sawa na asilimia 20 kutoka asilimia 7.0 mwaka 2011 kutokana na matokeo ya Utafiti Viashirikia vya UKIMWI na Malaria (THMIS) wa mwaka 2011/2012 hadi asilimia 5.6 mwaka 2016 kwa matokeo ya utafiti matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya UKIMWI (THIS) wa mwaka 2016/2017. Kiwango cha maambukizi ya VVU kwa wanawake ni asilimia 6.6 na wanaume ni asilimia 4.5 (THIS 2016/2017).
Katika utekelezaji wa malengo ya kitaifa ya kimkakati ya 95-95-95 (Tisini na Tano TaTu) kwa mwaka 2022, Makadirio ya idadi ya Watu Wanaoishi na Maambukizi ya VVU (WAVIU) katika Mkoa ni 63,088, ambapo wanawake ni 38,716 na wanaume ni 24,372. Kufikia robo ya Julai - Septemba 2022, 95 ya Kwanza; watu 60,862 kati ya WAVIU 63,088 sawa na asilimia 96.5 wamepimwa na kutambua hali zao za maambukizi ya VVU. 95 ya Pili; watu 60,133 kati ya WAVIU 60,862 wanaotambua hali zao za maambukizi ya VVU sawa na asilimia 98.8, wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs). Na 95 ya Tatu; watu 57,367 kati ya WAVIU 60,133 wanaotumia dawa za ARV sawa na asilimia 95.4, wamefubaza makali ya VVU. Utekelezaji wa malengo ya Kitaifa ya Kimkakati ya 95-95-95 kwa halmashauri umeainishwa katika jedwali namba 48:
Jedwali Na 48: kuonyesha Utekelezaji wa Malengo ya Kitaifa ya Kimkakati ya 95-95-95 kwa Halmashauri kwa mwaka 2022 kufikia Robo ya Tatu, Julai - Septemba.
Halmashauri |
Idadi ya WAVIU |
95 ya Kwanza |
95 ya Pili |
95 ya Tatu |
Maoni |
Madaba DC
|
3,536 |
112.6 |
98.5 |
96.3 |
Malengo yamefikiwa
|
Mbinga DC
|
7,841 |
105.8 |
98.8 |
95.4 |
Malengo yamefikiwa
|
Mbinga TC
|
7,620 |
88.9 |
98.9 |
95.7 |
95 ya kwanza haijafikiwa
|
Namtumbo DC
|
7,533 |
62.2 |
98.9 |
94.8 |
95 ya kwanza na 95 ya tatu havijafikiwa
|
Nyasa DC
|
5,525 |
122.9 |
98.5 |
94.3 |
95 ya Tatu haijafikiwa
|
Songea DC
|
5,730 |
105.7 |
98.6 |
95.6 |
Malengo yamefikiwa
|
Songea MC
|
16,776 |
99.6 |
99.6 |
96.1 |
Malengo yamefikiwa
|
Tunduru DC
|
8,528 |
88.8 |
97.5 |
94.5 |
95 ya kwanza na 95 ya tatu havijafikiwa
|
Jumla Mkoa
|
63,088 |
96.3 |
98.8 |
95.4 |
Malengo yamefikiwa
|
Chanzo cha Taarifa: DHIS-2, 10 Desemba, 2022.
Pamoja na mfanikio haya, Mkoa kupitia Timu ya Usimamizi na Uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa (RHMT) imejipanga kuendelea kufanya yafuatayo ili kufikia adhma ya malengo ya 95-95-95 kwa kila mwaka na 0-0-0 (Sifuri Tatu) ifikapo mwaka 2030:
6.3.2 Huduma za Ustawi wa Jamii
6.3.2.1 Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (iCHF)
Mkoa wa Ruvuma unatekeleza Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa kwa mujibu wa Waraka Na.1 wa Mwaka 2018 wa Maboresho ya Mfuko wa Afya ya Jamii ambao umeleta tija kubwa kwa wananchi katika kupata huduma za afya za uhakika. Hadi kufikia 30 Novemba, 2022 jumla ya kaya 25,745 (7.4%) zimeandikishwa kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (iCHF).
Jedwali Na.49: Hali ya iCHF Mkoa wa Ruvuma hadi 30 Novemba, 2022
NA
|
HALMASHAURI
|
IDADI YA KAYA
|
KAYA ZILIZOSAJILIWA
|
ASILIMIA
|
MAKUSANYO
|
1
|
MADABA DC
|
12,250
|
1,636
|
13.4%
|
49,080,000.00 |
2
|
MBINGA DC
|
57,738
|
4,965
|
8.5%
|
148,950,000.00 |
3
|
TUNDURU DC
|
82,129
|
6,659
|
8.1%
|
199,770,000.00 |
4
|
MBINGA TC
|
33,256
|
2,579
|
7.8%
|
77,370,000.00 |
5
|
NAMTUMBO DC
|
45,856
|
3,488
|
7.6%
|
104,640,000.00 |
6
|
SONGEA DC
|
33,933
|
2,510
|
7.4%
|
75,300,000.00 |
7
|
SONGEA MC
|
57,640
|
2,549
|
4.4%
|
76,470,000.00 |
8
|
NYASA DC
|
37,367
|
1,359
|
3.6%
|
40,770,000.00 |
|
JUMLA
|
360,169
|
25,745
|
7.4%
|
772,350,000.00 |
6.3.2.2 Usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya Miaka Mitano (U5BR)
Mkoa unaendelea kutekelezwa mpango wa usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano bure ulioanza Machi, 2020 katika Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma. Usajili na utoaji vyeti hufanywa na Wauguzi kwenye vituo vyote vya huduma za afya vinavyotoa huduma za afya ya mama na mtoto.
Lengo la Mkoa wa Ruvuma ni kusajili na kuwapatia vyeti watoto 242,140, ambapo hadi tarehe 30 Novemba, 2022 Mkoa umesajili na kutoa vyeti kwa watoto 242,083 (99.9%).
6.3.3 Huduma za Lishe
Katika kuendelea na kupambana na tatizo la utapiamlo nchini hususani udumavu (asilimia 41, TNNS 2018), Mkoa wa Ruvuma unatekeleza viashiria mbalimbali vilivyoainishwa katika mkataba wa Lishe ulioingiwa baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Utekelezaji wa mkataba kwa mwaka 2020/2021 Mkoa wa Ruvuma ulikuwa ni mshindi wa pili kitaifa na mwaka 2021/2022 Mkoa umeshika nafasi ya 4 Kitaifa. Matokeo haya kwa kiasi kikubwa yametokana na; -
Matumizi ya Kifungu/Lengo Y (Objective Y) katika kutekeleza shughuli zisizo za Lishe.
Kutumia vifungu/malengo mengine (objectives) kutekeleza shughuli za Lishe.
Haya yote yaliyotajwa hapo juu yamesababisha Mkoa kutofanya vizuri katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika mwaka wa fedha 2021/2022. Hivyo, ili kutekeleza Mkataba wa Lishe kwa Kiwango kinachotakiwa tunapendekeza yafuatayo; -
Waweka hazina wa Halmashauri wahakikishe vifungu vya Lishe (Objective Y expenditure codes) vinatumika kulipia shughuli za lishe tu
Maafisa Mipango wahakikishe vifungu vya Lishe vinatumika kupanga shughuli za Lishe tu
Maafisa Lishe wa ainishe vifungu sahihi vya shughuli anayokwenda kutekeleza.
Wakaguzi wa ndani ya Halmashauri wahakikishe wanafanya uhakiki wa fedha za lishe kila robo mwaka ili kubaini changamoto mapema na kuzitatua kwa wakati.
Aidha, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Mkoa kupitia Halmashauri zake umeendelea kutekeleza afua mbalimbali ikiwemo utengaji na utoaji wa fedha kwa ajili kutekeleza afua za lishe, ambapo jumla ya TZS. 355,274,918.3 zimepangwa na hadi kufikia Novemba, 2022 jumla ya TZS. 122,852,599 sawa na asilimia 34.6 tu zimetolewa kutekeleza afua za lishe katika Halmashauri kama inavyoonesha katika jedwali namba 50.
Jedwali Na. 50: Matumizi ya fedha zilizopangwa kutekeleza afua za lishe kwa Halmashauri katika mwaka wa fedha 2022/2023
NA
|
HALMASHAURI
|
FEDHA ILIYOTUMIKA JULAI - NOVEMBA, 2022 IKILINGANISHWA NA FEDHA ILIYOPANGWA MWAKA 2022/2023 |
KIASI CHA FEDHA KILICHOPANGWA KWA MTOTO (PER CAPITA PLANNED) FY 2022/2023 |
|||
KILICHOPANGWA |
KILICHOTUMIKA HADI NOVEMBA, 2022 |
% |
IDADI YA WATOTO |
TZS |
||
1
|
SONGEA MC
|
39,860,000 |
24,404,000 |
61.2 |
32216 |
1237 |
2
|
MBINGA TC
|
23,971,068 |
7,526,000 |
31.4 |
20961 |
1144 |
3
|
SONGEA DC
|
38,729,712 |
6,570,000 |
17.0 |
21396 |
1810 |
4
|
MBINGA DC
|
92,711,750 |
37,140,000 |
40.1 |
41575 |
2230 |
5
|
TUNDURU DC
|
71,204,134 |
21,254,600 |
29.9 |
47833 |
1489 |
6
|
NAMTUMBO DC
|
39,432,000 |
5,070,000 |
12.9 |
36712 |
1074 |
7
|
NYASA DC
|
23,823,206 |
11,744,000 |
49.3 |
27023 |
882 |
8
|
MADABA DC
|
25,543,048.3 |
9,143,999 |
35.8 |
7684 |
3324 |
JUMLA KUU
|
355,274,918.3 |
122,852,599 |
34.6 |
235400 |
1509 |
NB: - Halmashauri saba (7) ziliweza kupanga kwa kufuata kigezo cha kima cha chini cha TZS. 1000 kwa kila mtoto chini ya miaka mitano, isipokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ambayo ina jumla ya Watoto wenye umri chini ya miaka mitano 27023 lakini wamepanga TZS. 23,823,206 badala ya kima cha chini cha TZS. 27,023,000. Athari ya hii itafanya Halmashauri kutofikia matumizi ya kima cha chini cha TZS. 1000 wakati wa tathmini na mwisho wa siku itaathiri matokea ya Mkoa Kitaifa.
Ushauri: Tunapoelekea kwenye re–allocation Halmashauri ihakikishe inafanya marekebisho ili kuepuka hii changamoto kama iliyojitokeza mwaka wa fedha 2021/2022.
6.3.3.1 Mambo yanayosababisha lishe duni ni: -
Ulaji duni wa chakula unaotokana na kula milo michache na kiasi kisichotosheleza mahitaji ya virutubishi mwilini, hii pia hujumuisha kutowanyonyesha watoto ipasavyo.
Magonjwa ya mara kwa mara yanayoondoa hamu ya kula na, kusababisha ufyonzaji duni wa virutubishi na huongeza mahitaji ya virutubishi mwilini.
Matumizi mabaya ya chakula mfano kuuza chakula chote, kutumia nafaka kutengenezea pombe nk.
Utayarishaji mbaya wa chakula unaopoteza virutubishi kama kuosha mboga za majani baada ya kukatakata.
Upungufu katika matunzo ya makundi maalumu (watoto wadogo, wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, wazee na wagonjwa) Makundi haya yanahitaji matunzo na huduma muhimu za kiafya kama vile chanjo, kupata vidonge vya nyongeza, kutibu maradhi na huduma za kilishe.
Utapiamlo huathiri afya, uzalishaji mali na maendeleo katika jamii. Athari hizi hujitokeza katika hali ya kuchelewa kwa hatua za ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili, kuongezeka kwa magonjwa na vifo vya watoto, kupungua kwa kinga mwili na kupungua kwa uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji mali.
Hivyo, katika kuhakikisha jamii inaondokana na tatizo hili la lishe Halmashauri na Mkoa ni muhimu kuendelea kuelekeza nguvu katika kusimamia utekelezaji wa mikataba ya lishe ngazi ya Halmashauri, kata na vijiji / Mitaa ili jamii iweze:-
kubadili tabia na kuzingatia ulaji unaofaa.
Kupata elimu sahihi ya lishe kwa kupitia njia mbalimbali kama vyombo vya habari vilivyopo, ngoma za asili, viongozi wa dini na kimila.
Kupata elimu sahihi ya lishe katika kipindi cha siku 1000 za uhai wa mtoto (yaani toka mimba ilipotungwa hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka 2) –
Kuimarisha maadhimisho ya siku za afya na Lishe ya Kijiji zinazofanyika kila baada ya miezi mitatu.
Mkoa na Halmashauri kuhakikisha fedha inayotengwa kwa shughuli za lishe inatolewa na kufanya shughuli za lishe kama zilivyotengwa.
Mkoa na Halmashauri kuendelea kufanya usimamizi shirikishi ili kuweza kutambua changamoto zinazojitokeza kwa wakati na kuzitafutia ufumbuzi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.