Taarifa ya mifugo mkoani Ruvuma.docx,
Katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Mifugo Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuboresha huduma za ugani, uzalishaji wa mifugo, uendelezaji wa nyanda za malisho kwa mfumo wa ranchi ndogo, utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo, uboreshaji wa miundombinu ya mifugo, masoko ya mifugo pamoja na miundombinu ya udhibiti wa magonjwa ya mifugo kama ifuatavyo:-
Mkoa wa Ruvuma una watumishi wa ugani 109 wa mifugo na uvuvi kati ya watumishi 677 wanaohitajika. Idadi hiyo ya maafisa ugani inaufanya mkoa kuwa na upungufu wa maafisa ugani mifugo 568 kwa mchanganuo wa ufuatao:-
Jedwali Na. 31 Idadi ya Maafisa Mifugo mkoa wa Ruvuma
|
Idadi ya Maafisa Mifugo |
|
||||||||
|
Sekretarieti ya Mkoa |
Tunduru DC |
Nyasa DC |
Songea DC |
Madaba DC |
Mbinga DC |
Mbinga Mji |
Namtumbo DC |
Songea Manispaa |
Jumla |
Mahitaji
|
3 |
157 |
84 |
64 |
35 |
100 |
73 |
66 |
95 |
677 |
Waliopo
|
2 |
16 |
18 |
9 |
8 |
16 |
7 |
14 |
19 |
109 |
Upungufu
|
1 |
141 |
66 |
55 |
27 |
84 |
66 |
52 |
76 |
568 |
Waliopo kwenye mpango wa kuajiriwa
|
0 |
0 |
95 |
14 |
15 |
0 |
66 |
16 |
25 |
231 |
Pamoja na upungufu huo wa maafisa ugani Mkoa unaendelea kutoa huduma za ugani kwa kuwatumia maafisa ugani waliopo kuhudumia wastani wa vijiji 5 badala ya kijiji kimoja.
Ili kuimarisha ufugaji wa kisasa wa kuku pamoja na kuongeza uzalishaji wa kuku na mayai, Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi inategemea kuwa na mashamba darasa ya kufugia kuku katika Manispaa ya Songea ambapo vikundi vitatu (3) vya wafugaji wa Kuku vitapokea vifaranga wa Kuku 4,000 aina ya Sasso. Vikundi hivi vitajengewa miundombinu ya kufugia kuku pamoja na kupewa vyakula na madawa ya kutunza kuku kwa mwezi mmoja, kuku watakaofugwa watatumika kwa ajili ya kujifunzia ufugaji wa kuku na kugawa kwa vikundi vingine vya ufugaji kuku.
Athari za kupungua kwa malisho zimeendelea kujitokeza mara kwa mara kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na mifugo, mabadiliko ya tabia ya nchi na mtazamo wa wafugaji kutegemea malisho ya asili tu. Athari hizo zimesababisha mifugo kudhoofika na wakati mwingine kufa kwa kukosa malisho na maji.
Katika jitihada za kukabiliana na athari hizo, Wizara imeandaa mpango wa kuwajengea uwezo wafugaji kuzalisha, kutunza na kuhifadhi malisho kupitia utaratibu wa mashamba darasa ya malisho katika maeneo ya malisho. Katika utekelezaji wa mpango huu kazi zote zitakazohitaji nguvu kazi zitafanywa na vikundi vya vijana waliopo kwenye maeneo husika. Lengo la mpango huu ni kubadili mtazamo wa wafugaji kutegemea malisho ya asili tu na kuboresha maeneo ya malisho yaliyopo. Wizara imepanga kuanzisha mashamba darasa ya malisho 9 yenye jumla ya ukubwa wa ekari 45 katika Halmashauri za Wilaya za Madaba, Songea, Namtumbo na Tunduru. Lengo kuu la mpango huu ni kuwajengea uwezo wafugaji kuzalisha, kutunza na kuhifadhi mbegu na malisho kwa kutumia utaratibu wa mashamba darasa.
Mkoa wa Ruvuma una mifugo 3,354,927 idadi hiyo inajumuisha ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Nguruwe, Kuku, Bata, Punda, Mbwa na mifugo mingine midogo midogo kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na 32.
Jedwali Na. 32 Idadi ya Mifugo
|
TUNDURU |
NAMTUMBO |
MBINGA DC |
NYASA |
SONGEA DC |
MADABA |
SONGEA MC |
MBINGA TC |
JUMLA |
Ng’ombe |
68,440 |
50,853 |
36,856 |
22,290 |
27,307 |
17,766 |
5,405 |
6,211 |
235,128 |
Mbuzi |
30,235 |
54,465 |
102,563 |
39,585 |
37,665 |
6,648 |
4,992 |
17,208 |
293,361 |
Kondoo |
8,206 |
4,162 |
9,481 |
4,911 |
3,651 |
576 |
107 |
2,765 |
33,859 |
Nguruwe |
4,135 |
5,949 |
100,591 |
41,653 |
48,653 |
8,560 |
3,237 |
19,932 |
232,710 |
Kuku |
316,355 |
199,248 |
346,660 |
160,083 |
254,841 |
79,315 |
810,229 |
264,243 |
2,430,974 |
Bata |
17,386 |
2,708 |
4,105 |
3,985 |
3,867 |
2,504 |
1,125 |
2,311 |
37,991 |
Bata mzinga |
|
- |
- |
- |
91 |
21 |
36 |
23 |
171 |
Kanga |
2,357 |
127 |
2,391 |
- |
15,041 |
29 |
- |
241 |
20,186 |
Sungura |
523 |
253 |
423 |
- |
621 |
178 |
103 |
123 |
2,224 |
Njiwa |
|
1,905 |
8,408 |
- |
1,142 |
1,786 |
- |
251 |
13,492 |
Punda |
81 |
197 |
57 |
12 |
457 |
52 |
151 |
6 |
1,013 |
Mbwa |
2,725 |
5,051 |
13,781 |
6,257 |
4,642 |
4,998 |
2,296 |
3,213 |
42,963 |
Paka |
359 |
1,029 |
5,898 |
1,367 |
721 |
835 |
378 |
268 |
10,855 |
Kwa kipindi cha mwezi Julai, 2021 hadi Septemba 2022 uzalishaji wa mazao yatokanayo na Mifugo umefikia tani 3,555.41 za nyama ya ng’ombe, mbuzi na kondoo, tani 1,732 za nyama ya nguruwe tani 2010.79 na tani 603 za nyama ya kuku. Uzalishaji wa maziwa umefikia lita 1,120,807.2 wakati uzalishaji wa mayai umefikia mayai 29,439,196, vipande vya ngozi za ng’ombe zilizozalishwa ni 22,572, vipande vya ngozi za mbuzi na kondoo ni 19,500.
Mkoa wa Ruvuma umeendelea na shughuli za udhibiti wa magonjwa ambapo kwa kipindi cha Mwezi Julai 2021 hadi Septemba, 2022 magonjwa yaliyojitokeza zaidi ni Ndigana kali, Ndigana baridi, Homa ya Mapafu kwa ng’ombe na mbuzi, ugonjwa wa Mapele ngozi, Kideri na homa ya matumbo kwa kuku na Ndui.
Ili kukabiliana magonjwa ya Mifugo, Mkoa umesimamia utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ambapo Ng'ombe 6,273 wamepatiwa chanjo dhidi ya Homa ya Mapafu (CBPP), mbwa 8,749 na paka 38 wamepatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha Mbwa (Rabies), Kuku 182,327 dhidi ya Ugonjwa wa Kideri, ugonjwa wa Ndui na ugonjwa wa Gumboro.
Katika utekelezaji wa zoezi la uogeshaji wa mifugo michovyo 118,590 imefanyika kwa kipindi cha mwezi Julai, 2021 hadi Septemba, 2022.
Matokeo ya uogeshajikatika Mkoa wa Ruvuma ni kupungua kwa vifo vya mifugo vitokanavyo na magonjwa yaenezwayo na kupe na ndorobo.
Pamoja na jitihada hizi katika zoezi la uogeshaji mifugo kuna changamoto ambazo ni pamoja na;
Kwa sasa Mkoa kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejenga Majosho 11 katika Halmashauri za Tunduru majosho tisa (9), Songea DC Josho moja (1) na Nyasa Josho moja (1) kwa thamani ya Tshs 246,000,000.00. Hata hivyo mkoa umeendelea kushikirikiana na Wizara na kupitia bajeti ya mwaka 2022/2023 unategemea kujenga Majosho mapya 2 katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwenye Kijiji cha Njalila Kata ya Mgazini na Kijiji cha Nambendo Kata ya Ndongosi kwa thamani ya Tshs. 44,000,000.00
Mkoa una mbwa 43,919 ambao wako wanaofugwa kisasa na wengine wanaofugwa kiholela. Kufuatia kuwepo kwa idadi kubwa ya mbwa wanaozurura mitaani na kuwa kero kwa ustawi na afya ya jamii inayotuzunguka, kumekuwa na jitihada za kuchanja mbwa ili kudhibiti ugonjwa huu unaoathiri wanyama na binadamu kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Septemba, 2022 mbwa 8,749 walichanjwa. Pia kumekuwepo na matukio 172 ya mbwa kung’ata binadamu. Pamoja na juhudi hizo Mkoa unaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa, kampeni ya uchanjaji mbwa, na kuua mbwa wote wanaozurura ili kuendelea kuilinda jamii dhidi ya ugonjwa huu.
Mkoa ulipokea dozi 1000 za chanjo ya kichaa cha Mbwa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuadhimisha wiki ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa na kutoa elimu ya ufugaji wa kisasa wa mbwa. Wiki hiyo iliadhimishwa kuanzia tarehe 26 Septemba 2022 hadi tarehe 02 Oktoba 2022 ambapo mbwa 2,717 walichanjwa.
6.1.3.6 Utekelezaji wa Uboreshaji Miundombinu ya Masoko na Biashara ya Mifugo
Uongezaji Thamani Zao la Maziwa
Pia katika jitihada za kuimarisha mnyororo wa thamani wa maziwa, Mkoa umefanya uchunguzi wa ugonjwa wa kutupa mimba (brucelosis) kwa ng’ombe wa maziwa 104 katika Halmashuri ya Mbinga Mji.Mkoa unaendelea kuhamasisha wafugaji zaidi waweze kupima ng’ombe zao ili kuzuia maambukizi zaidi.
Kwa upande wa usindikaji wa Maziwa Mkoa una wasindikaji wadogo 6 wanaosindika wastani wa lita 201,600 kwa mwaka. Aidha ,ili kuimarisha lishe kwa jamii wananchi wanaendelea kuhamasishwa kunywa maziwa ili kufikia lengo la unywaji wa lita 200 za maziwa kwa kila mtu kwa mwaka.
Minada ya Mifugo na Uongezaji Thamani Zao la Nyama
Mkoa kwa kushirikiana na Bodi ya Nyama ulifanya ukaguzi wa mabucha 156 na machinjio 6 za nyama ya ng’ombe na nguruwe katika Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Mbinga MjI ili kumlinda mlaji na kuhakikisha kuwa bucha zote zinasajiliwa na kukidhi vigezo vya kuuza nyama bora. Wafanayabishara wote walipewa muda wa miezi sita (6) kufikia Disemba 2022 wawe wameanza kutumia Misumeno ya kukatia nyama na magogo ya Plastiki ili kuhakikisha kuwa nyama inakuwa na ubora unaotakiwa.
Pia Mkoa una viwanda viwili vya kusindika nyama katika Abbasia ya Peramiho na Chipole Sisters Halmashauri ya Wilaya ya Songea maarufu kwa usindikaji wa sausages za nyama wastani wa tani 100 za nyama kwa mwaka.
Katika kuimarisha biashara ya Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo Mkoa una Mnada mmoja (01) wa upili katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Kijiji cha Mtyangimbole na minada sita (06) ya awali katika kijiji cha Ruanda (Mbinga), Lituhi Nyasa, Muhuwesi (Tunduru), Mhepai (Songea), Ligera na Lismonji (Namtumbo) kwa ajili ya kufanyia biashara ya mifugo
Mkoa katika kujidhatiti na upatikanaji wa malisho bora ya mifugo na kuepusha migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi na kuboresha mahusiano kati ya wakulima na wafugaji Mkoa umefanya mambo yafuatayo: -
Kwa mwaka 2021/2022 zoezi la upimaji na uandaaji wa vitalu limefanyika katika kijiji cha Litowa na Magwamila katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambapo hekta 13,110.493 zimepimwa.
Hata hivyo kumekuwepo na ongezeko la mifugo inayochungwa holela katika maeneo kadhaa ya Mkoa yakiwemo mashamba ya wakulima na katika hifadhi za Taifa na misitu ya kijamii, na waliopangiwa kwenye vitalu kutoka kwenye maeneo hayo. Hali hiyo imejitokeza zaidi katika Wilaya ya Namtumbo na Tunduru. Hii imesababisha wakulima kuamua kulinda mazao yao ili yasiharibiwe au kuliwa na mifugo na hivyo hatua hiyo inayochukuliwa na wakulima imekuwa ikileta kutoelewana baina ya wakulima na wafugaji na wakati mwingine kusababisha matukio ya kuchukua sheria mkononi na kupelekea kujeruhiana.
Aidha, kwa mifugo iliyoko kwenye hifadhi imekuwa ikisababisha tembo kukimbia kwenye hifadhi na kwenda kwenye makazi ya watu na hivyo kusababisha uharibifu wa mali za wananchi na wakati mwingine maafa yamekuwa yakitokea.
Hata hivyo Mkoa umechukua hatua za kukutana na viongozi wa wafugaji kwa ajili ya kutatua changamoto hii, ambapo moja ya maelekezo kwa wafugaji kupitia viongozi ni kuwataka wafugaji kukaa katika maeneo waliyopangiwa na kuwa na mifugo kuendana na eneo walilo nalo.
Pia kuzielekeza Halmashauri zenye wafugaji kutatua changamoto ya ukosefu wa miundombinu kwenye maeneo yaliyotengwa kwa kushirikiana na wafugaji kujenga majosho, malambo na visima vya maji ili wafugaji wabakie katika maeneo yao waliopangiwa, Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru katika mwaka wa fedha 2021/2022 ilikusanya kiasi cha Tshs. 190,423,000.00 kupitia adhabu mbalimbali kwa wafugaji wanaokiuka taratibu ikiwa ni pamoja na kulisha kwenye vyanzo vya maji na nje ya maeneo ya kufugia.
Mfumo wa Utambuzi na Ufuatiliaji Mifugo Tanzania unasimamiwa kwa Sheria ya Usajili, Utambuzi na Ufuatiliaji Mifugo Na.12 ya Mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011 na Kwa Mkoa wetu wa Ruvuma Halmashauri ziko kwenye hatua tofauti ya kutekeleza zoezi hili. Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Mkoa wametoa elimu ya kwa Wahe. Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara za Mifugo na Uvuvi, Maafisa Tehama na Maafisa Utambuzi wa Halmashauri.
Faida ya zoezi hili la utambuzi ni; Kusaidia Kudhibiti wizi wa mifugo, Kuthibitisha umiliki wa mifugo hiyo, Fursa ya kibiashara kimataifa kwa kukidhi viwango, ushindani, na matakwa ya soko la kimataifa, Uhakika wa usalama wa chakula kwa kuifahamu idadi ya mifugo na jinsi ya kuvuna mifugo hiyo na mazao yake, pia itasaidia kuepusha migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Aidha, kupitia matangazo ya Serikali Taarifa kwa Umma kupitia hotuba ya Mhe. Waziri Mkuu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zoezi la utambuzi limesitishwa mpaka hapo Serikali itakapofanya Tathmini na kutoa maelekezo. Mpaka zoezi linasitishwa Mkoa ulikuwa umefanya utambuzi kwa mbuzi na kondoo 875, Ng’ombe na punda 5,539 katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Namtumbo, Songea, Mbinga Mji na Manispaa ya Songea.
Kuhimiza matumizi ya kinga zaidi kuliko tiba kwa mifugo;
Kuendelea kuhamasisha ujenzi wa miundombinu ya mifugo;
Kutoa elimu ya ufugaji wa kisasa wenye tija; na
Kuhamasisha uanzishaji wa viwanda vidogo vya kusindika mazao ya mifugo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.