JARIDA la madini mkoani Ruvuma.pdf
2 Biashara
Kufanyika kwa Mabaraza ya Biashara
Mabaraza ya Biashara ya Wilaya na Mkoa hufanyika kwa Mujibu wa waraka wa Rais Na.1 wa mwaka 2001, ikiwa ni jukwaa la Majadiliano kati ya Sekta binafsi na Sekta ya Umma ambapo Baraza la Biashara la Mkoa lilifanyika tarehe 21 Disemba, 2021 na kupitia Mabaraza ya Biashara changamoto mbalimbali huibuliwa na kufanyiwa kazi. kwa sasa hamasa inaendelea kutolewa kwa viongozi wa Wilaya na Halmashauri kuitisha mabaraza ya biashara kwa ngazi ya Wilaya kwa kuwa ni jukwaa muhimu linalokutanisha Sekta binafsi na Sekta ya Umma kwa ajili ya Majadiliano.
Upangaji wa machinga katika maeneo rasmi ya kufanyia biashara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wakati ikizindua Mpango wa uelimishaji na uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022, alielekeza kuwapanga machinga na zoezi hilo, lifanyike kwa umakini kwa lengo la kuepuka vurugu, fujo na uonevu. Ambapo Mkoa wa Ruvuma kupitia maekelezo hayo tulianza kutekeleza.
Hali ya utekelezaji wa maelekezo ya upangaji wa Machinga.
Kuunda Uongozi wa Machinga kwa ngazi ya Mkoa na ngazi ya Halmashauri kwa kuwa Mkoa wa Ruvuma haukuwa na uongozi wa machinga.
Kuwaunganisha Viongozi wa Machinga Mkoa na Viongozi wa Machinga Taifa na kushiriki semina mbalimbali za Viongozi wa Machinga zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika Dodoma.
Halmashauri zimetenga maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Machinga.
Kuendelea kutoa Vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo.
Viongozi wa Machinga kuwezeshwa na Mkoa na Halmashauri kufanya ziara kwenye Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kujitambulisha, kutoa elimu ya Katiba na Kanuni za Shirikisho na kuhamasisha machinga kuhamia kwenye maeneo rasmi yaliyotengwa na Halmashauri.
Halmashauri zimeendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya masoko na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za Machinga.
Changamoto zilizojitokeza wakati wa upangaji wa Machinga
Baadhi ya Wafanyaboiashara kukataa kufanya biashara kwenye maeneo yaliyotengwa.
Miundombinu mbambali kwenye baadhi ya masoko ambapo Machinga wanafanyia biashara imechakaa inahitaji kufanyiwa marekebisho.
Baadhi ya machinga kurejea kufanya biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi.
Baadhi ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za machinga kutokuwa na Miundombinu muhimu,
Utoaji wa Leseni za Biashara
Mkoa unaendelea na zoezi la kurasimisha Biashara na kutoa Leseni kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utoaji wa Leseni za Biashara kama Serikali ilivyo Agiza. Mwaka 2021/2022 jumla ya Leseni 7,815 zilitolewa na kupata jumla ya TShs 722,254,500 zilikusanywa ikiwa ni mapato ya ndani yatokanayo na utoaji wa Leseni za Biashara katika Mkoa wa Ruvuma. Jedwali namba 38 hapa chini linaonesha Idadi ya Leseni zilizotolewa kwa kila Halmashauri.
Jedwali Na. 38: Idadi ya leseni zilizokatwa kwa kila halmashauri mwaka 2021/2022
Na.
|
Halmashauri
|
JULAI, 2021 – JUNI, 2022 |
|
Idadi ya Leseni |
Thamani |
||
1 |
SONGEA MC
|
2,681 |
327,737,000
|
2 |
MBINGA TC
|
1290 |
150,364,000
|
3 |
MBINGA DC
|
376 |
23,885,000
|
4 |
MADABA DC
|
383 |
24,350,000.
|
5 |
TUNDURU
|
1798 |
96,594,000.
|
6 |
SONGEA DC
|
213 |
21,354,000
|
7 |
NYASA DC
|
485 |
37,647,000
|
8 |
NAMTUMBO
|
589 |
40,323,500
|
|
JUMLA
|
7,815 |
722,254,500
|
Fursa za Uwekezaji Mkoani Ruvuma
Mkoa wa Ruvuma una fursa za Uwekezaji katika Sekta za Kilimo, Biashara, Ufugaji, Misitu, Madini, Utalii, Mawasiliano, Umeme wa Maporomoko ya Maji, Uvuvi, Viwanda, Uendelezaji wa Makazi, Usafiri na Usafirishaji ambapo fursa zote hizi zimeanishwa kwenye Mwongozo wa Uwekezaji uliozinduliwa tarehe 25 Julai, 2019 katika viwanja vya Majimaji mjini Songea. Mkoa unaendelea kupokea Wawekezaji mbalimbali ambao wanaonesha nia ya kuwekeza Mkoa wa Ruvuma
6.2.3 Taarifa ya Timu ya Kuchambua, Kuandaa na Kuanisha Mfumo Mzuri wa Uwajibikaji Kwa Jamii (CSR) wa Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Ruvuma
6.2.3.1 Utangulizi
Lengo mahususi la ripoti hii ni kuelezea hali halisi ya Uwajibikaji kwa Jamii wa wachimbaji wa Madini waliopo Mkoa wa Ruvuma. Hii ni kufuatia Timu ambayo iliundwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuchambua, kuandaa na kuainisha mfumo mzuri wa Uwajibikaji kwa Jamii (Corporate Social Responsibility), kazi ambayo timu ilipewa kuifanya kwa muda wa wiki sita.
Lengo mahususi la kuundwa kwa Timu hiii ilikuwa ni kuhakikisha, inapata taarifa za wachimbaji wa Madini jinsi wanavyowajibika kwa jamii, pia kujifunza kwenye Mikoa yenye uchimbaji wa Madini namna wanavyotekeleza na kusimamia wachimbaji wa Madini juu ya Uwajibikaji kwa Jamii kwa kuchangia utekelezaji wa Miradi ya maendeleo. Baada ya hapo, kuchambua, kuandaa na kuainisha mfumo mzuri wa CSR ambao utatumika kwenye Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma. Kazi hii imefanyika, imekamilika na kuwasilishwa kwa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Ruvuma, Mheshimiwa Kanali Laban Elias Thomas
Jedwali Na. 39: Wajumbe wa Timu
Na.
|
JINA
|
WADHIFA
|
TAASISI ANAYOTOKA
|
CHEO
|
1
|
Amos Samwel Lugomela
|
Mwenyekiti
|
TAKUKURU
|
Afisa Uchunguzi Mkuu Kiongozi
|
2
|
Joseph Martin Kabalo
|
Katibu
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
|
Afisa Biashara Mkoa
|
3
|
E 9476 SGT Kheri Said Komagi
|
Mjumbe
|
Jeshi la Polisi
|
Askari Polisi
|
4
|
Edmund Eslom Lubinga
|
Mjumbe
|
Usalama wa Taifa
|
Afisa Usalama
|
5
|
Zabron Paul Walwa
|
Mjumbe
|
TRA
|
Afisa Mkuu Msimamizi wa Kodi
|
6
|
Dickson Francis Mbugano
|
Mjumbe
|
Ofisi ya Madini
|
Mhandisi Migodi
|
7
|
Frank John Chonja
|
Mjumbe
|
Ofisi ya Taifa ya Mashitaka
|
Wakili wa Serikali
|
6.2.3.3 Hadidu za Rejea
Kutafuta taarifa za utekelezaji wa CSR katika Mikoa na sehemu mbalimbali zenye uchimbaji na biashara ya Madini.
Kupata na kupitia mapato ya mwaka (Annual turnover) ya Makampuni yanayochimba madini/yanayofanya biashara ya madini.
Kupata na kuchambua Mipango ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR Plans) ya Makampuni husika.
Kuangalia na kulinganisha mipango (CSR Plans) ya Makampuni na utekelezaji wa mipango hiyo.
Kuanisha na kubainisha Makampuni ya uchimbaji madini yamefanya nini/yametekeleza mpango gani katika jamii hadi sasa.
Kupata maoni ya wadau wa madini na kujadili nao juu ya namna bora ya kutekeleza mipango ya uwajibikaji kwa jamii (CSR Plans) katika Mkoa wa Ruvuma.
Kuandaa mfumo wa utekelezaji wa mipango ya uwajibikaji kwa jamii kwa kushirikiana na Makampuni ya uchimbaji na biashara ya madini.
Kufanya kazi zingine zinazohusiana na zitakazosaidia kuandaa mfumo fanisi wa utekelezaji wa mipango ya uwajibikaji kwa jamii (CSR Plans).
Kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mipango ya uwajibikaji kwa jamii.
6.2.3.4 Namna Timu Ilivyofanya Kazi
Kukutana na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na kupata maelekezo ya namna ya kufanya kazi kwa kuzingatia hadidu za rejea.
Timu kukutana, kutambulishana, kupitia hadidu za rejea na kuandaa mpango kazi.
Kupitia Sheria ya Madini Sura Na. 123 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019, kifungu cha 105.
Kuomba taarifa za mauzo (turnover) za wachimbaji wote wa madini waliopo Mkoa wa Ruvuma pamoja na orodha ya wachimbaji Mkoa wa Ruvuma.
Timu ilikutana na Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya zilizopo Mkoa wa Ruvuma pamoja na Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya ili kupata maoni yao namna ya utekelezaji wa Uwajibikaji kwa jamii wa wachimbaji wa madini.
Timu ilikwenda katika Halmashauri za Wilaya ya Songea, Mbinga, Nyasa, Namtumbo na Tunduru kwa lengo la kukutana na viongozi wa Halmashauri na kamati za Serikali za Vijiji na kuomba taarifa na kupata maoni yao juu ya utekelezaji wa CSR.
Timu ilikwenda kujifunza katika Mikoa ya Shinyanga na Geita namna zinavyotekeleza Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) katika Halmashauri za Wilaya ya Msalala, Geita, Halmashauri ya Mji Geita na Manispaa ya Kahama.
The Mining Act Chapter 123 Revised Edition 2019
105.(1)A Mineral right holder shall on annual basis, prepare a credible corporate social responsibility plan jointly agreed by the relevant local government authority or local government authorities in consultation with the Minister responsible for local government authorities and Minister responsible for Finance.
(2) The plan prepared under subsection (1) shall take into account environmental, social, economic and cultural activities based on local government authority priorities of host community.
(3) The corporate social responsibility plan referred to under subsection (1) shall be submitted by a mineral right holder to a local government authority for consideration and approval.
(4) Subject to the provision of this section, every local government authority shall;-
(a) Prepare guidelines for corporate social responsibility within their localities;
(b) Oversee the implementation of corporate social responsibility action plan; and
(c) Provide awareness to the public on projects in their areas
(5) In this section “host community” means inhabitants of the local area in which mining operations activities take place.
6.2.3.6 Aina za Madini Yanayopatikana Katika Mkoa wa Ruvuma
Mkoa wa Ruvuma umebarikiwa kuwa na madini aina mbalimbali ambayo yanaweza kuunufaisha Mkoa wa Ruvuma endapo kutakuwa na usimamizi mzuri na kuhakikisha Wachimbaji wanawajibika kwa jamii kwa utaratibu mzuri.
Ifuatayo ni orodha ya aina ya madini na maeneo yanapopatikana.
Jedwali Na.40: Orodha za Aina ya madini yanayopatikana katika Mkoa wa Ruvuma
Na.
|
Aina ya Madini
|
Mahali yanapopatikana
|
1
|
Dhahabu
|
Nyasa (Darpori, Mpepo na Nindi)
Mbinga (Mhongozi na Lukalasi) Namtumbo (Kitanda) Tunduru (Mbesa na Mbati) |
2.
|
Shaba
|
Nyasa (Mt. Livingstone)
Mbinga (Ndongosi) Tunduru ( Mbesa na Mbati) |
3
|
Makaa ya Mawe
|
Nyasa (Liweta na Malini)
Mbinga (Luanda, Mbuyula na Paradiso) Songea (Mhukuru) |
4
|
Chuma
|
Namtumbo (Mtonya)
|
5
|
Urani
|
Namtumbo (Mtonya)
|
6
|
Madini ya Ujenzi na Viwanda (Mchanga, Kokoto, Moramu naMawe)
|
Nyasa
Mbinga Namtumbo Songea (Mhukuru na Mtyangimbole) na Tunduru |
7
|
Madini ya Vito (Sapphire, Ruby, Alexandrite,Chrisoberly,Spinel, Ganet,Aquamarine,Tourmaline)
|
Tunduru(Ngapa,Muhuwesi,Majimaji,Mbuyula na Lukala)
Nyasa( Maeneo ya Mwambao wa Ziwa) Mbinga (Maeneo ya Mkako, Masuguru,Ngembambili, Amani Makolo na Kuhagala) Namtumbo(Mputa,Lusewa,Suluti,Mtwarapachani,Mkongo na Kiburungutu) |
6.2.3.7 Hali ya Utekelezaji wa CSR Ndani ya Mkoa wa Ruvuma
Timu ilitembelea Halmashauri za Tunduru, Mbinga, Nyasa, Namtumbo na Songea zenye uchimbaji wa Madini na kubaini mambo yafuatayo;
Udhaifu mkubwa katika ufuatiliaji na utekelezaji wa CSR wa Makampuni yanayochimba Madini.
Halmashauri kukosa uelewa wa namna ya kusimamia CSR kutokana na wachimbaji wa Madini waliopo katika maeneo yao.
Miradi ya CSR kutekelezwa katika Vijiji vinavyozunguka maeneo ya uchimbaji pekee bila kuwa na tafsiri sahihi ya neno “Local area” kwenye sheria ya madini.
Halmashauri kutokuwa na mtu maalum anayehusika na CSR.
Halmashauri kutokuwa na Mwongozo, Hati ya Makubaliano (MoU) na Mpango wa Uwajibikaji wa wachimbaji wa Madini.
Katika maeneo ambayo CSR inatekelezwa haiendani na mauzo ya Madini kutoka kwa wachimbaji. Kwa mfano Ruvuma Coal Ltd iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, ilianza uchimbaji Mwezi April, 2020 hadi kufikia Januari 2022 walikuwa wamechimba na kuuza Makaa ya Mawe tani 1,023,567.85 zenye mauzo ya Tshs 104,007,680,959.46 na endapo wangechangia CSR hata asilimia 0.5 wangechangia Tshs 520,038,404.80 lakini hadi Machi, 2022 wamechangia Tshs 35,000,000 tangu waanze uchimbaji hii ni sawa na asilimia 0.033 ya mauzo.
Wachimbaji wa Madini kutoa fedha kwenye Vijiji kwa ajili ya kutekeleza miradi ya CSR, lakini miradi imekuwa ikitekelezwa kwa kusuasua. Kwa mfano Kampuni ya Ruvuma Coal Ltd ilitoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni Kumi (10,000,000/=) tangu mwaka 2020 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Sara kilichopo Mbinga DC lakini hadi kipindi timu inatembelea eneo hilo, mradi huo ulikuwa haujaanza kutekelezwa.
Halmashauri kushindwa kusimamia kikamilifu matakwa ya Sheria ya Madini kuhusiana na suala la CSR.
Baadhi ya wachimbaji wa Madini kutowajibika kwa jamii kwa kuchangia Miradi ya Maendeleo.
Wataalam wa Halmashauri kushindwa kufika kwenye maeneo ya miradi kwa wakati kwa lengo la kutoa ushauri na kutoa maelekezo ya taratibu za utekelezaji wa miradi. Ambapo ilibainika kuwa Kijiji cha Malini kilichopo Nyasa DC kiliingiziwa fedha na Kampuni ya Godmwanga Germs Ltd kiasi cha Shilingi Milioni kumi tangu mwezi Disemba, 2020 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati lakini wataalam kutoka Halmashauri hawajafika kwa ajili ya kutoa maelekezo ya kitaalam ya eneo la ujenzi na gharama za ujenzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ina Madini aina ya Mchanga na Gemstones na timu ilibaini kutokuwepo kwa takwimu za mauzo ya gemstones.
Halmashauri kushindwa kusimamia kikamilifu matakwa ya Sheria ya Madini kuhusiana na suala la CSR.
6.2.3.8 Miradi Iliyopangwa Kutekelezwa na Iliyotekelezwa na Wachimbaji wa Madini Ikiwa ni Sehemu ya Uwajibikaji kwa Jamii Ndani ya Mkoa wa Ruvuma
Timu ilitembelea Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma pamoja na baadhi ya wachimbaji kwa lengo la kuona hali ya utekelezaji na Uwajibikaji kwa Jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali kwenye maeneo hayo. Katika hatua hii, ilibainika kwamba wachimbaji walio wengi hawana Uwajibikaji kwa Jamii na timu ilifanikiwa kupata baadhi ya wachimbaji walio na mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii na utekelezaji wake. Wachimbaji hao kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo;
Jedwali 41: Wachimbaji Waliowajibika kwa Jamii kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma
Na.
|
H/Shauri
|
Jina la mchimbaji
|
Mwaka
|
Kiasi cha CSR
|
Utekelezaji
|
1
|
Mbinga |
Tancoal Enegy Ltd
|
2020/2021
|
80,300,000
|
22,800,000
|
Ruvuma Coal Ltd
|
2020/2021
|
60,000,000
|
15,000,000
|
||
2021/2022
|
45,000,000
|
15,000,000
|
|||
2
|
Songea DC
|
Lukolo Company Ltd
|
2017- 2019
|
11,833,320
|
11,833,320
|
3
|
Nyasa DC
|
Godmwanga Germs Ltd
|
2019/2020
|
4,050,000
|
14,050,000
|
4
|
Tunduru
|
Ruby International Ltd
|
2018
|
70,000,000
|
70,000,000
|
Elia Joseph Gikalo
|
2018
|
20,000,000
|
20,000,000
|
||
|
JUMLA
|
|
|
291,183,320
|
168,683,320
|
6.2.3.9 Wawekezaji Wengine Wanaowajibika kwa Jamii Nje ya Wachimbaji wa Madini
Wawekezaji hawa kwa mujibu wa Sera za Makampuni yao wanatambua Uwajibikaji kwa Jamii kutokana na shughuli wanazozifanya katika maeneo husika na wamekuwa wakitekeleza Uwajibikaji kwa Jamii japo si kwa kiwango kinachoridhisha.
Katika utekelezaji wa CSR kwa upande wa Mabenki, kila tawi limekasimiwa madaraka ya kupokea maombi toka kwenye jamii ya maeneo ilipo Benki kwa vipaumbele vya sekta ya Elimu na Afya, kisha maombi hayo huwasilishwa Makao Makuu kwa ajili ya kupitiwa na kuidhinishwa. Viwango vya CSR vinavyotolewa na taasisi hizo za fedha, NMB ni asilimia moja (1%) ya faida na Benki zingine hawakuwa na taarifa za viwango vya CSR kwa kuwa uratibu wake unafanywa Makao Makuu ya taasisi hizo.
Jedwali 42: Wawekezaji wengine nje ya wachimbaji wanaowajibika kwa Jamii
Taasisi
|
Mwaka
|
Kiwango cha CSR kilichotekelezwa
|
NMB
|
2019 - 2022
|
75,865,000.00 |
CRDB
|
2020/2021
|
77,000,000.00 |
NBC
|
2020/2021
|
Haijatekeleza |
TCB
|
2021
|
6,480,000.00 |
AVIV
|
2017- 2022
|
93,495,000.00 |
JUMLA
|
|
252,840,000.00 |
Timu ilifanya ziara ya kwenda kujifunza na kupata uzoefu katika Mikoa ya Shinyanga na Geita ambapo kuna uchimbaji mkubwa wa Madini ya Dhahabu. Katika Mikoa hiyo, timu ilitembelea Halmashauri ya Manispaa Kahama na Halmashauri ya Wilaya Msalala zilizopo katika Mkoa wa Shinyanga pia Halmashauri ya Mji wa Geita na Halmashauri ya Wilaya ya Geita zilizopo Mkoa wa Geita. Katika maeneo hayo, timu ilifanikiwa kuona mafanikio ya utekelezaji wa Uwajibikaji kwa Jamii wa wachimbaji wa Madini hasa upande wa wachimbaji wakubwa. Mambo ambayo timu imejifunza katika Mikoa hiyo juu ya utekelezaji wa CSR ni kama ifuatavyo;
Halmashauri zilianza maboresho ya CSR kuanzia mwaka 2018 kutokana na juhudi za Wakuu wa Mikoa kutaka kufanya maboresho kwenye eneo hilo. Hili lilifanyika baada ya kuongezwa kifungu namba 105 ndani ya sheria ya Madini Sura namba 123 kinachohusu CSR.
Halmashauri zilipitia Sheria kwa lengo la kupata ufahamu wa utekelezaji mzuri wa CSR, pamoja na maeneo mengine zilipata tafsiri ya neno “Local area” na kutanua wigo wa wanufaika wa CSR kwa mujibu wa tafsiri ya Sheria ya Madini Sura Na. 123 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019. Hivyo, utekelezaji wa CSR unahusisha maeneo yote ya Halmashauri na ngazi ya Mkoa.
Kila Halmashauri iliandaa Mwongozo wa Uwajibikaji kwa Jamii kwa kuzingatia sheria ya madini Sura Na. 123 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 kifungu cha 105(4)(a).
Kila Halmashauri iliteua waratibu wa CSR watakaohusika na masuala yote ya CSR.
Kufanya vikao vya maridhiano kati ya Halmashauri na wachimbaji wa Madini na kuwa na kiwango cha CSR cha asilimia 1 ya mauzo kwa mwaka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita na Mji Geita na kiwango cha asilimia 0.7 kwa Halmashauri ya Manispaa Kahama na Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Kuandaa Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR Plan), Hati ya Maridhiano (MoU) na kuunda kamati za kusimamia miradi.
Kwa mujibu wa Miongozo ya Halmashauri zipo Kamati za Uwajibikaji kwa Jamii ngazi ya Wilaya ambazo kazi yake ni kusimamia shughuli zote za CSR na kufanya vikao vyake kila mwezi na Wakurugenziwa Halmashauri wanagharamia vikao hivyo. Vilevile, yupo mratibu wa CSR ngazi ya Mkoa anayesimamia shughuli zote za CSR kwa Halmashauri zote.
Halmashauri za Mkoa wa Geita zinatekeleza miradi yake kwa utaratibu wa Mgodi kuingia Mkataba na watoa huduma na kuwasilisha vifaa kwenye Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi. Hivyo, kazi ya manunuzi na ulipaji wa fedha inafanywa na Mgodi na Halmashauri zinabaki kuwa wasimamizi wa ujenzi wa miradi na Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga zinasimamia hatua zote za manunuzi kwa njia ya nguvu ya pamoja (Force account) na kuwasilisha Nyaraka za madai kwa Wachimbaji kwa ajili ya malipo.
6.2.3.11 Utekelezaji wa Miradi ya CSR Kwenye Maeneo ya Halmashauri za Kahama, Msalala, Geita TC Na Geita DC
Timu iliweza kutembelea baadhi ya miradi na kupata taarifa za utekelezaji wa CSR katika Mikoa ya Shinyanga na Geita, ambapo miradi ya CSR katika maeneo hayo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutokana na mfumo mzuri ulioandaliwa na Mikoa hiyo. Utekelezaji wa miradi ni kama ilivyoainishwa katika majedwali hapo chini;
Jedwali Na. 43: Miradi iliyotekelezwa na gharama zake katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018 hadi 2021.
Mwaka
|
Idadi ya Miradi
|
Kiasi cha CSR (Tshs)
|
Thamani ya Miradi iliyotekelezwa (Tshs)
|
2018
|
25
|
5,004,007,955.00 |
5,310,223,409.30 |
2019
|
27
|
4,977,500,600.00 |
5,225,460,446.51 |
2020
|
47
|
4,645,000,000.00 |
4,154,307,300.00 |
2021
|
47
|
4,920,000,000.00 |
1,528,793,140.00 |
JUMLA
|
146
|
19,546,508,555.00 |
16,218,784,295.81 |
ii) Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Jedwali Na. 44: Miradi iliyotekelezwa na Gharama zake katika kipindi cha kuanzia mwaka 2020-2021
Mwaka
|
Idadi ya Miradi
|
Kiasi cha CSR (Tshs)
|
Thamani ya Miradi iliyotekelezwa (Tshs)
|
2020
|
31
|
4,300,000,000.00 |
3,495,630,217.00 |
2021
|
48
|
4,900,000,000.00 |
|
JUMLA
|
79
|
9,200,000,000 |
3,495,630,217.00 |
iii) Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Jedwali Na. 45: Miradi iliyotekelezwa na gharama zake katika kipindi cha kuanzia mwaka 2019/2020
Mwaka
|
|
Idadi ya Miradi
|
Kiasi cha CSR ( Tshs)
|
Thamani ya Miradi iliyotekelezwa (Tshs)
|
2019/2020
|
Awamu ya 1
|
58
|
2,294,371,653.00 |
1,392,144,801.00 |
Awamu ya 2
|
8
|
344,000,000.00 |
330,584,500.00 |
|
JUMLA
|
66
|
2,638,371,653.00 |
1,722,729,301.00 |
iv) Halmashauri ya Wilaya Msalala
Jedwali Na. 46: Miradi iliyotekelezwa na gharama zake katika kipindi cha kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.
Mwaka
|
Idadi ya Miradi
|
Kiasi cha CSR ( Tshs)
|
Thamani ya Miradi iliyotekelezwa (Tshs)
|
2019
|
12
|
515,773,000.00 |
497,961,260.00 |
2020
|
30
|
900,000,000.00 |
653,103,964.91 |
2021
|
20
|
2,530,000,000.00 |
468,605,728.28 |
JUMLA
|
62
|
3,945,773,000.00 |
1,619,670,953.19 |
6.2.3.12 Changamoto za Timu Wakati wa Utekelezaji wa Majukumu
Baadhi ya wachimbaji na Taasisi kuchelewa na wengine kushindwa kuwasilisha taarifa zao zilizohitajika kwenye timu.
Timu kushindwa kufika kwenye baadhi ya maeneo ya miradi kutokana na changamoto ya miundombinu ya barabara na muda.
Mjumbe mmoja wa timu kukosekana baadhi ya wiki katika utekelezaji wa majukumu ya timu kutokana na kupangiwa kazi nyingine na Mkuu wake wa Taasisi.
Halmashauri hazikuwa na watu maalum wa kutoa taarifa sahihi za utekelezaji wa CSR kwenye timu.
6.2.3.13 Maoni ya Timu
Suala la uwajibikaji kwa jamii kwa wachimbaji wa Madini ndani ya nchi ya Tanzania ni la kisheria, na kwa jinsi hiyo wachimbaji wote wa madini katika Mkoa wa Ruvuma wanapaswa kuendesha shughuli zao za uchimbaji na kulipa Uwajibikaji kwa Jamii ili jamii inayozunguka migodi inufaike na uwepo wa madini kutokana shughuli hizo za uchumi na athari za kimazingira.
Kwa kuwa timu hii imefanikiwa kwenda katika maeneo ya Kahama (Shinyanga) na Geita kwa ajili ya kujifunza na kupata uzoefu, uzoefu huo toka maeneo hayo unapaswa kutumika katika Mkoa wa Ruvuma kwa wachimbaji wote waliopo. Kazi ya kuweka kiwango cha uwajibikaji kwa jamii ni ngumu, inahitaji kuwa na meza ya mazungumzo kati ya Serikali ya Mkoa, Halmashauri na wachimbaji, lakini nguvu kubwa iwekwe kwenye ushawishi na mshikamano wa pamoja (upande wa Serikali na Taasisi zake) hususani katika kuweka kiwango cha CSR na utekelezaji wake.
Halikadhalika, eneo jingine la uwajibikaji kwa jamii ambalo Timu imelibaini ni Makampuni yaliyopo ndani ya Mkoa wa Ruvuma hususani taasisi za fedha (Benki) na Wawekezaji katika Sekta ya Kilimo. Hii ni kwa mujibu wa hadidu za rejea ambazo timu ilipewa. Timu imebaini kwamba Makampuni haya yamekuwa na uwajibikaji kwa jamii, lakini bado hakuna mfumo mzuri uliowekwa ili kuwa na kiwango halisi kinachotambulika pamoja na usimamizi wa Serikali. Ni Benki moja tu ya NMB iliyoweka wazi kuwa asilimia moja ya faida inayopatikana kwa mwaka huwa inatolewa ikiwa ni uwajibikaji kwa jamii. Hivyo maeneo haya nayo, timu ina maoni ya kwamba yawekewe mfumo mzuri wa uwajibikaji kwa jamii. Japo la kupendeza ni kwamba makampuni haya yana Sera/miongozo inayobainisha uwepo wa uwajibikaji kwa jamii wa Makampuni yao ili kunufanisha jamii na kuleta mahusiano mazuri katika jamii.
Kuteua Waratibu wa CSR ngazi ya Mkoa na Halmashauri ambao wataratibu shughuli zote za CSR pamoja na kuanzisha mchakato wa uboreshaji wa CSR Mkoa wa Ruvuma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iitishe kikao cha wadau wa Madini kwa lengo la kutoa elimu ya utekelezaji wa CSR kwa kuzingatia uzoefu uliopatikana katika Mikoa ya Geita na Shinyanga.
Mkoa ufanye vikao vya majadiliano na maridhiano na wachimbaji wa Madini ili kuwa na makubaliano ya pamoja ya kiwango cha CSR na namna ya utekelezaji wake.
Timu inapendekeza kiwango cha CSR kiwe kati ya asilimia 0.7 hadi asilimia 1 ya mauzo ya mwaka husika.
Tafsiri ya jamii inayozunguka mgodi ‘’Local area’’ kwenye sheria ya madini Sura 123 (R.E 2019) iwe eneo lote la Halmashauri na Mkoa.
Mamlaka za Serikali za Mitaa ziandae Miongozo ya Uwajibikaji kwa Jamii kama sheria ya madini inavyoelekeza.
Kila mchimbaji wa Madini awe anaandaa Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR Plan) kwa kila mwaka.
Halmashauri ziwe na jukumu la kusimamia mwenendo wa utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kupitia CSR bila kupokea fedha kwa miradi inayotekelezwa na wachimbaji wenye Makampuni ya kigeni. Kwa Makampuni ya ndani utaratibu uwekwe wa namna ya kuwa na Mfuko wa pamoja wa CSR utakaosimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Wakurugenzi waunde Kamati za CSR kwenye maeneo yao.
Zitungwe Sheria ndogo ambazo zitawabana wasafirishaji wanaomwaga Makaa ya Mawe barabarani kwa lengo la kuzuia uharibifu wa mazingira.
Kuboresha mawasiliano kwenye taasisi zote za Serikali zinazosimamia Madini kama Tume ya Madini, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi.
Wataalam wa Halmashauri kusimamia hatua zote za utekelezaji wa miradi ya CSR kwa kushirikiana na wachimbaji ili kuwa thamani ya fedha.
Halmashauri zenye madini zipimwe utendaji kazi wake kwa jinsi zinavyotekeleza miradi ya CSR.
MoU ibainishe hatua ambazo zitachukuliwa kwa wachimbaji watakaoshindwa kutekeleza Uwajibikaji kwa Jamii.
Kamati za CSR zitoe elimu kwa wananchi na wachimbaji juu ya Sheria ya Madini na namna CSR inavyotakiwa kutekelezwa.
Kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa taarifa za Madini yanayouzwa ili kuweza kutoza ushuru wa huduma (Service Levy), CSR na mapato mengineyo kwa uhalisia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ishauri Mamlaka inayohusika ili Sheria ya Madini Sura ya 123 (R.E 2019) itengenezewe kanuni itakayoonesha kiwango cha CSR.
Utaratibu wa utekelezaji wa CSR utumike pia nje ya wawekezaji wa Madini.
Chombo cha uchunguzi TAKUKURU ichukue hatua za kisheria kufanya uchunguzi ili kubaini matumizi ya fedha shilingi milioni kumi (10,000,000.00) kwa Kijiji cha Sara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kilichotolewa na Kampuni ya mgodi ya Ruvuma Coal kwa mwaka 2020 kwa kuwa kuna viashiria vya ubadhirifu.
Timu inampongeza Mkuu wa Mkoa Ruvuma, Mheshimiwa Kanali Laban Elias Thomas kwa kusimamia kazi hii hadi kukamilika na hatimaye kufikia hatua ya kuanza kuandaa mfumo mzuri wa uwajibikaji kwa jamii wa wachimbaji wa madini Mkoa wa Ruvuma. Kazi ya timu hii imefanyika kwa weledi, uaminifu, uadilifu na kwa bidii kwa lengo la kutimiza azma ya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa. Ni wajibu wa kila mdau katika Mkoa wa Ruvuma kutoa ushirikiano wa dhati ili kufikia azma hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.