• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

AMCOS zote kufungiwa mizani ya kieletroniki

Imewekwa kuanzia tarehe: July 20th, 2022

Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa stakabadhi ghalani nchini Asangye Bangu amesema wanatarajia kuimarisha matumizi ya mizani ya kieletroniki katika vyama vyote vya msingi ili kupunguza changamoto ya tofauti ya malipo ambayo imekuwa inalalamikiwa na wakulima wakati wa malipo.

Amesema mizani ya kieletroniki inaonesha namba bila utata kwa wakulima na kwamba mizani hiyo imeanza kugawiwa katika mikoa inayonunua mazao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ikiwemo Mkoa wa Kagera ambao tayari umepelekewa mashine zaidi ya 180.

"Uzuri wa mashine za kieletroniki ikisoma uzito unaingia moja kwa moja kwenye kazi data na kutoa karatasi yenye data zote badala ya kuandikwa kwa mkono",alisema Bangu.

Akizungumza na wakulima wa Chama cha Msingi cha Ushirika Nanyumbu mkoani Mtwara amesema Ofisi yake pia inaimarisha matumizi ya TEHAMA kwenye mfumo huo ili kuondoa kero kwa wakulima kwenye mfumo wa malipo.

Amesema katika ziara yake ya kutembelea wakulima kwenye vyama vya Msingi amepata malalamiko kuhusiana na changamoto chache zinazotokea kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani.

Hata hivyo amesema wakulima wanaukubali mfumo huo hivyo wameshauri changamoto hizo zipatiwe ufumbuzi ili mfumo huo uwe na tija kubwa kwa wakulima.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu  Baraka Mlangwa amesema wakulima wanafaidika kutokana kutumika mfumo wa stakabadhi ghalani hasa katika mazao ya ufuta na korosho .

Amesema wananchi wanauza mazao yao kwa bei nzuri na kuna Usalama wa kutosha wa fedha zao kwa sababu malipo yanapitia benki.

Kwa upande wake Afisa Ushirika wa  Wilaya ya Nanyumbu Daniel Mlungu ameyataja makusanyo ya ufuta msimu huu kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa yamefikia zaidi ya tani 2200 na kwamba kilo moja ya ufuta imefikia shilingi 3000.

Baadhi ya wakulima wa AMCOS ya Nanyumbu wamepongeza mfumo huo kutumika kwa wakulima ambao wameutaja kuwa na faida nyingi ukilinganisha na hasara.

Mzee Hamisi Lilangunda amesema mfumo wa stakabadhi ghalani umewaokoa kutoka mfumo wa uuzaji mazao holela ambao ulokuwa una mnyonya mkulima kwa miaka mingi.

Said Mpopera ameomba changamoto za kuchelewa kwa malipo kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani zitafutiwe ufumbuzi sanjari na kuchelewa kwa pembejeo za kilimo katika zao la korosho kuna punguza uzalishaji wa zao hilo ambalo linategemewa na wakulima wengi.

Mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara ndiyo mikoa inayoongoza kwa matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani hali ilyosababisha wakulima kupata tija kwenye kilimo.
imeandikwa na Albano Midelo

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.