Na Gustaph Swai-RS Ruvuma
Naibu Waziri wa Afya, Mheshimiwa Dr. Godwin Mollel, ameeleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya.
Akizungumza wakati wa ibada ya kumsimika Abate mpya wa Peramiho iliyofanyika katika Kanisa la Peramiho, Dr. Mollel amesema kuwa kwa asilimia 97, serikali imewezesha huduma za kiteknolojia za afya zinazotolewa Ulaya na India kupatikana katika hospitali zilizopo hapa nchini.
"Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya afya amefanya uwekezaji mkubwa, ameshakamilisha asilimia 97 ya teknolojia tuliyokuwa tunaifuata Ulaya na India tayari iko kwenye nchi yetu," alieleza Dr. Mollel
Naibu waziri ameitaja teknolojia hiyo kuwa na uwezo wa kurahisisha huduma za upasuaji kama vile uvimbe chini ya sakafu ya ubongo, kifua, moyo, mgongo, na huduma kwa watoto wanaozaliwa na seli mundu ambapo huduma zote hizo sasa zinatolewa nchini.
Sanjari na hayo Naibu Waziri ameeleza umuhimu wa lishe bora katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa chakula lakini inakabiliwa na tatizo la lishe na udumavu.
Ametoa wito kwa viongozi wa dini kuwasaidia wananchi kutambua umuhimu wa lishe bora ili kuimarisha afya ya jamii na kuweza kuchangia maendeleo katika Taifa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile ameitaja hospitali ya Rufaa ya Peramiho inayoongoza katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Kusini kwa kuhudumia wagonjwa wengi wa figo kwa wakati mmoja.
Katika juhudi za kuunga mkono sekta ya afya, Naibu Waziri wa Afya ameeleza kuwa serikali imedhamria kuondoa vikwazo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta ya afya nchini, hususan katika masuala ya kodi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.