MWENYEKITI wa bodi ya mamlaka ya usimamizi wa wanyapori Tanzania(Tawa)Meja Jenerali Mstaafu Hamisi Semfuko,amewaonya wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kutoka mamlaka hiyo kutofanya ubabe kwa wananchi wanaokwenda kuwatumikia.
Badala yake, amewataka wahitimu hao kuwa wakakamavu,kushirikiana na jamii na kufanya kazi kwa weledi mkubwa wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Meja Jenerali Semfuko,ametoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya Kijeshi kozi namba 16 kutoka mfumo wa kiraia kwenda mfumo wa kijeshi katika Chuo cha mafunzo ya Uhifadhi maliasili kwa jamii(CBCTC) Likuyu Sekamaganga kilichopo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
“askari unatakiwa kuwa mkakamavu,ukipita kijijini kila mtu akufahamu kama wewe ni askari kutokana na ukakamavu wako,kuonyesha ukakamavu siyo kuonyesha ubabe,lazima tutofautishe ukakamavu na ubabe”alisema Semfuko.
Aidha,ameitaka jamii kuhakikisha wanashirikiana na askari wa uhifadhi katika masuala mbalimbali ikiwemo kudhibiti wanyama wakali na waharibifu wanaovamia makazi yao na kuharibu mazao.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo mafunzo ya Uhifadhi maliasili kwa jamii(CBCTC) Likuyu Sekamaganga Jane Nyau alisema,kumekuwa na matukio mengi ya askari wa wanyamapori kulalamikiwa na wananchi kwamba katika utendaji wa kazi zao kuna uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.
Alisema kuwa, mara kwa mara askari wa uhifadhi wananyooshewa vidole katika utekelezaji wa majukumu yao kwa madai ya kutozingatia haki za binadamu,jambo ambalo ni kinyume kwa kuwa katika mafunzo yao hawafundishwi uvunjifu wa haki za binadamu au kutesa wananchi.
Naye Kamishina msaidizi mwandamizi wa mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (Tawa) Yusufu Kabange,ametoa tahadhari kwa wananchi kuhusiana na wanyama wakali na waharibifu hasa tembo wanaovamia makazi yao na kuwauwa.
Alisema,kwa kawaida matukio hayo yanatokea majira ya alfajiri na usiku ambapo amewataka wananchi kuacha kufanya shughuli zao au kutembea wakati huo ili kuepuka madhara ya kuvamiwa na wanyama.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.