• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ASKARI WANYAMAPORI 37 wahitimu mafunzo Namtumbo

Imewekwa kuanzia tarehe: November 14th, 2022

ASKARI wanyamapori wa vijiji(VGS)37,wamehitimu mafunzo maalum ya kozi namba 18/2022  katika chuo cha mafunzo ya Uhifadhi Maliasili kwa Jamii Likuyusekamaganga wilaya ya Namtumbo mkoni Ruvuma.

Akitoa taarifa ya mafunzo hayo,Mkuu wa chuo hicho Jane Nyau alisema,askari hao wamepata mafunzo maalum ya mbinu za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu ikiwa ni utekelezaji wa mkakati huo.Alisema,mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa wiki mbili chini ya ufadhili wa  Mamlaka ya usimamizi Wanyamapori Tanzania(Tawa)na wahitimu hao wametoka katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Nyau alisema,askari hao  wamejifunza mbinu ambazo ni rahisi kuzitumia katika mazingira yao ya kawaida ambazo hazitumii gharama kubwa kiuendeshaji na zinawapatia faida nyingine mbadala.

Alitaja baadhi ya faida hizo ni kutumia mizinga ya nyuki ambayo mbali na kudhibiti wanyamapori hasa Tembo,lakini wananchi watanufaika kwenye kilimo kwani nyuki hao  huhusika katika uchavushaji wa maua na hivyo kuongeza mazao kwa wakulima,wananchi kupata chakula ikiwamo asali na nta.

Alisema,matarajio ya chuo  kwamba askari hao watakaporejea kwenye maeneo yao watakwenda kupunguza migogoro kati ya wanyamapori na binadamu kwa kushiriki moja kwa moja kuwadhibiti na kutoa elimu kwa jamii kuhusu mbinu walizofundishwa ili waweze kuzitumia kutatua changamoto hizo.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mamlaka ya udhibiti wa wanyamapori Tanzania(Tawa)Kamishina msaidizi Said Mshana alisema, kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Tawa imepanga kuchimba mabwawa 50 ya maji katika Hifadhi mbalimbali za Taifa.

Alisema,mpango wa kuchimba mabwawa hayo ni mkakati wa kudhibiti  na kupunguza mtawanyiko wa wanyamapori wakali na waharibifu  kwenda nje ya maeneo yao.

Alisema mkakati mwingine ni kuongeza doria za udhibiti wanyamapori pori wakali na waharibifu,ambapo jumla ya  doria 64,724 zimefanyika katika kipindi cha Julai hadi Juni 2022 na kujenga vituo 16 vya kudumu vya askari wa kudhibiti matukio  ya wanyamapori katika wilaya 16 hapa nchini.

Mshana alisema, hatua hizo na nyingine zilizopangwa kutekelezwa naTawa zitasaidia kupunguza changamoto ya mara kwa mara inayotokea ya wanyama hao kutoka kwenye hifadhi kwenda kwenye makazi ya watu na kusababisha uharibifu  mkubwa wa mazao mashambani.

Kwa mujibu wa Mshana,matukio ya migongano kati ya wanyamapori na wananchi yanayoongezeka  kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na binadamu kuendesha shughuli zao kwenye mapito na mtawanyiko,na hivyo kupelekea ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Kamishina Mshana,amewakumbusha wananchi wanaokaa jirani na maeneo ya hifadhi,kutofanya shughuli  zozote za kibinadamu katika maeneo hayo,ili kuepuka  madhara yanayoweza kutokea.

Mkuu wa wilaya ya Nantumbo Dkt Julius Ningu,ameipongeza Tawa kwa kuchukua hatua madhubuti katika kudhibiti matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu  ambao wanatishia maisha na mali za wananchi.

Alisema,hatua hizo pamoja na kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa kusimamia utatuzi wa migogoro baina ya watu na wanyamapori wa mwaka 2020-2024.

Alisema,mkakati huo unaohusisha wadau mbalimbali ikiwamo taasisi za uhifadhi,NGO’s na Halmashauri za wilaya utawezesha kupunguza migogoro na muingiliano kati ya wanyapori na binadamu.

Amewapongeza wahitimu kwa uvumilivu walioonyesha katika kipindi chote cha mafunzo na kueleza kuwa,mafunzo waliyoyapata yamewajengea utimamu wa mwili na kuwapatia mbinu za udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu.

Katika risala yao iliyosomwa na Nassoro Ndengwike wahitimu hao walisema,  katika kipindi cha mafunzo  wamefundishwa mbinu mbalimbali za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu,uhifadhi wa maliasili zilizopo katika hifadhi za Taifa,sheria za uhifadhi,fidia na vifuta jasho.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.