• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ASKOFU awakumbusha watanzania umuhimu wa kulinda amani

Imewekwa kuanzia tarehe: October 4th, 2022

ASKOFU Mkuu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dkt Donald Mtetemela,amewataka viongozi wa Dini nchini kujiepusha na kauli na vitendo vitakavyopandikiza chuki na uchochezi kwa waumini wao dhidi ya  Serikali na dini nyingine.

Askofu Mtetemela ametoa kauli hiyo jana,wakati wa Ibada ya kumweka wakfu na kumsimika Kasisi Noel Mbawala kuwa Askofu wa kwanza wa Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi(KIUMA)lililopo kijiji cha Milonde kata ya Matemanga wilaya ya Tunduru.

Ibada  hiyo imeongozwa na Mhashamu Baba Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania na Dayosisi ya Tanga Maimba Mndolwa kwa niaba ya Makanisa ya Jumuiya ya Kikiristo Tanzania (CCT)  baada ya kanisa hilo kujiunga rasmi na jumuiya hiyo.

Aidha Dkt Mtetemela,amewataka viongozi wa dini hapa nchini,kushirikiana  na kuheshimu mamlaka za serikali ili  kuendelea kutunza amani na mshikamano uliopo badala ya kuwa chanzo cha mfarakano na migogoro isiyokuwa na manufaa kati ya waumini,serikali na jamii kwa ujumla.

“ili  mtu uwe kiongozi  nzuri ni muhimu  sana kushirikiana na serikali iliyopo madarakani,kuwa na maono,dira ,na mahusiano  kwa waumini wako na wale wa dini nyingine,kiongozi asiye na mahusiano na maono kamwe hawezi kufanikiwa katika nafasi yake”alisisitiza Askofu Mtetemela.

Amewakumbusha viongozi na waumini kuwa,katika mifarakano na uhasama wowote ndani ya kanisa  hakuna atakayeibuka mshindi bali wote watakuwa watu tulioshindwa.

Dkt Mtetemela amesisitiza,kiongozi nzuri siyo anayefanya maamuzi bila kuwashirikisha wengine,bali ni  mwenye kushirikisha wenzake, na waumini wa dini nyingine na kulisaidia kanisa kuibua vyanzo na miradi mingi ya maendeleo.

Amewaasa viongozi kuacha tabia ya kung’ang’ania madaraka ili kuepusha migogoro na migongano inayoweza kuwagawa waumini wao na kuhatarisha uhai na usalama wa kanisa.

“mara kadhaa tumeshuhudia migogoro na mapigano kwenye makanisa watu wakigombea madaraka na mali,nawakumbusha viongozi kufuata misingi na taratibu ziliowekwa na ikiwamo kuachia madaraka pindi muda unapokoma”alisisitiza Dkt Mtetemela.

Dkt Mtetemela,amewataka viongozi wa dini na Serikali kuwa na hofu ya Mungu, kauli nzuri kwa watu walio chini yao,kujiepusha na wizi na kujilimbikizia mali kwani kufanya hivyo itapelekea kutoamini na kuheshimika kwa waumini  wao na jamii.

Amewaomba waumini wa kanisa hilo,kushirikiana na viongozi wao na kuzika(kusahau)tofauti za nyuma na kulisaidia kanisa,kutunza mali ili ziweze kuwafikia wahitaji  wenye matatizo na shida mbalimbali.

Katika hatua nyingine Dkt Mtetemela,amempongeza mwasisi wa Kanisa hilo Dkt Matomoro Matomora na familia ya Profesa Diechmann ya Ujerumani ambayo imetumia sehemu ya mapato yake kuanzisha  kanisa na taasisi ya Kiuma ambayo imekuwa na mchango mkubwa kupunguza tatizo la umaskini,afya na elimu kwa Watanzania.

Mwakilishi wa familia ya Profesa Diechmann ambayo ndiyo  mfadhili wa kanisa hilo Susanna Diechamann alisema,familia inafarijika kuona misaada wanayotoa kwa kanisa na la Upendo Kristo Masihi  na taasisi ya Kiuma inatumika vizuri na kuhaidi kuendelea kushirikiana katika kutoa huduma kwa kanisa na huduma za kijamii.

Amempongeza Askofu Mbawala kwa kusimikwa kuwa kiongozi wa Kanisa hilo ambapo alieleza kuwa,hatia hiyo inalifanya kanisa la Upendo wa Kristo Masihi sasa kuwa na uongozi  baada ya kuondoka kwa mwasisi wa kwanza Dkt Matomora Matomora.

Amemtaka Askofu Mbawala na watumishi wengine wa Taasisi ya Kiuma,kuhakikisha fedha zote zinazoletwa zinatumika kama ilivyokusudiwa ili kuimarisha huduma za kanisa na za kijamii kama elimu na afya.

Kwa upande wake Askofu  wa kanisa la Upendo wa Kristo Masihi(KIUMA)Askofu Noel  Mbawala,amehaidi kuwatumikia vyema waumini wa kanisa hilo,kujifunza,kusimamia misingi na malengo ya  kanisa,kushirikiana na waumini na Serikali  iliyopo madarakani.

Kwa mujibu wa Askofu Mbawala ni kwamba, umoja na ushirikiano kati ya kanisa,waumini na serikali ndiyo utakao msaidia katika kuendesha  na kuongoza taasisi ya KIUMA ambayo tangu ilipoanzishwa imekuwa na mchango mkubwa kwa watu wa mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla.

Aidha,ameipongeza serikali kwa kuimarisha  na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii ikiwamo ujenzi wa barabara  ya lami kutoka Mbambabay-Mbinga-Songea hadi Tunduru.

Alisema,kuimarika kwa huduma za kijamii hasa barabara hiyo imesaidia  sana hata watumishi wanaoletwa kufanya kazi katika wilaya ya Tunduru kutofikiria kuhama kutokana na mazingira mazuri yaliyopo kwa sasa.

Hata hivyo,ameiomba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwapatia watumishi hasa wa sekta ya afya ili waweze kuongeza nguvu na kupunguza changamo ya uhaba wa wataalam kwenye Hospitali ya KIUMA.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amehaidi kuwa,serikali itaendelea kushirikiana na kuzitegemea taasisi za dini kujenga misingi imara ili kudumisha amani miongoni mwa Watanzania.

Alisema,serikali itaendelea kuheshimu uhuru wa watu wake kuabudu dini wanayoamini  kwa sababu ni moja kati ya haki za msingi za kila mwananchi kwa mujibu wa Katiba ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na itafanya kila iwezalo kuhakikisha uhuru huo unaheshimiwa.

Alisema,uhuru wa kuabudu ni nyenzo muhimu iliyowezesha Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kote Ulimwenguni ambapo amehaidi serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini zote ili kuhakikisha uhuru wa kuabudu hauchezewi na mtu au kikundi chochote.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.