Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea Mhashamu Damian Dallu ametoa onyo kali kwa jamii na viongozi juu ya masuala ya rushwa katika uchaguzi na matumizi mabaya ya madaraka.
Mhashamu Dallu ametoa onyo hilo wakati anahubiri kwenye adhimisho la misa takatifu ya kumsimika na kumbariki Abate mpya wa Peramiho, Mhashamu Emanuel Mlwilo OSB iliyofanyika katika Kanisa la Abasia ya Peramiho Jimbo Kuu la Songea.
"Inawezekana tatizo halipo kwa watu hawa wanaochaguliwa, Sasa rushwa imeingia katika jamii, bila kupokea rushwa hakuna raha, mtakosa wale ambao wanataka wawasaidie" alisisitiza Mhashamu Dallu.
Amekemea tabia ya rushwa licha ya kwamba ni dhambi na kwamba inaathiri uchaguzi, na kuchangia kuleta viongozi wasiofaa ambao hawana nia ya kutumikia jamii bali kufaidika kwa kutoa rushwa.
Ameonya kuwa kuendeleza tabia ya kupokea rushwa itaiumiza serikali kwa kuwa italeta viongozi wasiofaa, ambao hawawezi kuwatumikia watu bali kuwanufaisha viongozi wanarushwa.
Ameongeza kuwa uongozi unapaswa kuwa na ridhaa ya watu wa jamii, na kwamba kiongozi anayechaguliwa lazima awe ni mtu anayefahamika na jamii kwa uwezo wake na tabia yake.
Katika hatua nyingine Askofu Mkuu Dallu amewasihi viongozi wa dini na wale wenye mamlaka serikalini kutotumia vibaya madaraka yao badala yake wawe wanyenyekevu na kuwatumikia wale waliowachagua.
Kauli ya Askofu Dallu imekuja wakati ambapo jamii inajiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika nchini Novemba 27,2024 na uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani ambao unatarajia kufanyika mwaka 2025.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.