wananchi wametakiwa kulinda miundombinu ya umeme kwa kuepuka shughuli za uchomaji moto kwenye maeneo ya mashamba yao ambayo yamezunguka nguzo za umeme kwani kwakufanya hivyo kunaweza kuathiri kukosekana kwa huduma ya umeme katika maeneo mengine
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Judith Kapinga, Mara baada yakuwasha umeme kwa mara ya kwanza katika kijiji cha Mpingi Kata ya Matimila Halimashauri ya Songea
Kapinga ameeleza kuwa maendeleo ni hatua na lazima yawe na awamu ambapo hadi hivi sasa kwa Mkoa wa Ruvuma umebakiza vijiji viwili tu kati ya 554 na kwa Tanzania nzima ni chini ya vijiji 151, ili kukamilisha katika hatua ya awali ya kupeleka umeme kwenye ngazi ya vijiji na baadae kusambaza kwenye vitongoji vyote.
Ametumia nafasi hiyo kumtambulisha Mkandarasi Kampuni ya MF ambae hivi karibuni ataanza kutekeleza mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 284 vya Mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza awali wakati akitoa taarifa kuhusu mradi huo wakupeleka umeme katika kijiji hicho cha Mpingi Kata ya Matimira , Mhandisi Kutoka REA Robert Dulle, ameeleza kuwa mradi umegharimu takribani milioni 149 mpaka kukamilika kwake huku akitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo wajitokeze kwa wingi kuunganishiwa umeme.
Naye Diwani wa Kata ya Matimira ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Mheshimiwa Menas Komba, ametoa shukrani zake za dhati kwa wakala wa Umeme Vijijini REA, kwa kufikisha huduma hiyo kijijini hapo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.