• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BAKWATA walivyodhamiria kutoa elimu ya maadili nchi nzima

Imewekwa kuanzia tarehe: August 1st, 2023

KUTOKANA  na kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili kwa jamii hapa nchini ikiwemo matendo  ya ubakaji na ushoga,Baraza kuu la waislamu Tanzania(Bakwata)limeanza kuzunguka nchi nzima kutoa elimu na kukemea matendo hayo kwa waumini wake na kuishi kwa kufuata mafundisho ya Dini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Da’awa na Tabligh kutoka Baraza  kuu la Waislamu Tanzania(Bakwata) Sheikh Arif Surya,wakati akizungumza na waumini wa Kiislam  baada ya kukamilisha Ibada ya Ijitimai iliyoambatana na Dua maalum ya kuliombea Taifa katika msikiti Mkuu wa wilaya ya Tunduru.

Ibada hiyo imefanyika kwa siku tatu ambapo viongozi  kutoka Baraza la Waislamu(Bakwata)wilaya ya Tunduru na  Bakwata makao makuu wamezunguka katika vijiji mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu na mafundisho kwa waumini wao.

Shekhe Surya alisema,lengo la ibada hiyo ni muendelezo wa viongozi wa Dini ya Kiislam wakiongozwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt Abubakar Zuber,kukemea matendo maovu yanayoanza kushamiri kwa kasi kubwa hapa nchini ambayo ni kinyume na mafundisho ya dini hiyo na maagizo ya MwenyeziMungu.

Shekhe Surya alisema,baadhi ya watu kutoka mataifa ya nje wanafanya jitihada kubwa zinazokwenda kinyume na maadili na mafundisho ya MwenyeziMungu kwa kuwafundisha watoto wa kiume kujiingiza kwenye ndoa za jinsia moja.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro,ametoa wito kwa viongozi wa Dini,viongozi wa kimila na wazazi wilayani humo kutumia sehemu ya muda wao kuzungumza na watoto na vijana.

Alisema,hatua hiyo itasaidia sana kupunguzana na kukomesha vitendo vya ukiukaji wa maadili vinavyoendelea kufanywa na baadhi ya watu hapa nchini.

Alisema,vijana wakifundishwa vizuri mila,desturi na kushika mafundisho ya dini na wakawa na hofu ya Mwenyezi Mungu maovu mengi ikiwemo ndoa za jinsia moja,ulawiti na unyanyasaji wa kijinsia vitapungua kwa kiwango kikubwa hapa nchini.

Aliongeza kuwa,serikali itaendelea kushirikiana na Dini zote katika kujenga maadili mema kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla,hata hivyo amewaomba viongozi hao kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan ili aweze kutekeleza vema mipango ya maendeleo katika nchi yetu.

Aidha,Mkuu wa wilaya ametumia nafasi hiyo kukemea vikali vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto wa kike na kiume  na kuhaidi kwamba serikali ya wilaya itahakikisha inaongeza nguvu katika kupambana na ukatili na kuimarisha ulinzi kwa watoto hao.

Amewakumbusha viongozi wa dini wilayani humo, kuendelea kukemea vitendo vyote vinavyoweza kuwagawa Watanzania ikiwemo tofauti za Dini kwa kuwa sisi sote ni wamoja na kuwapongeza viongozi hao kwa kuendelea kudumisha amani,umoja na mshikamano.

Mtatiro amewasa wazazi na walezi kuweka mifumo imara ya ulinzi kwa watoto  kuanzia ngazi ya familia,mtaa,mashuleni na sehemu nyingine ili kulinda haki na ustawi wa watoto na kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya watu wazima katika jamii.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Bakwata wilayani Tunduru Abdala Kawanga,ameishukuru serikali kwa kuendelea kushirikiana na viongozi wa Dini hali iliyowezesha wilaya hiyo kuwa na utulivu na wananchi kupata muda wa kufanya shughuli zao za uzalishaji mali.

Amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,kupeleka mbolea za bure kwa wakulima wa zao  maarufu la korosho na kuhaidi waumini wa Kiislam wataendelea kumuunga mkono katika jitihada za kuleta maendeleo hapa nchini.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.