• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BANDARI ya Mbamababay kuunganisha Reli ya Kusini

Imewekwa kuanzia tarehe: February 25th, 2024

Na Albano Midelo,Mbambabay

NAIBU Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa David Kihenzile amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 70 kuanza  uboresha bandari ya Mbambabay ziwa Nyasa mkoani Ruvuma.

Amesema mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo ni miezi 24 na kwamba Mkandarasi amekabidhiwa eneo la mradi Januari 26,2024 na kwamba kukamilika kwa mradi kutaongeza uwezo wa kuhudumia shehena ya mizigo kwa bandari hiyo kutoka tani 110,000 hadi 550,000 kwa mwaka.

“Uboreshaji wa bandari hiyo ni maandalizi ya  kuanza mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR  ukanda wa kusini kutoka Mtwara hadi Mbambabay mkoani Ruvuma  na kuunganisha Liganga na Mchuchuma mkoani Njombe’’,alisisitiza.

Ameitaja nia ya serikali ni kuhakikisha kwamba  reli ya kutoka Mtwara hadi Mbambabay inajengwa na kwamba kazi inayofanywa na serikali hivi sasa ni kuhakikisha  inatafutwa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa reli hiyo.

Amesisitiza kuwa mradi huo utakapokamilika utatoa fursa ya usafirishaji katika ushoroba wa Mtwara na nchi za Maziwa Makuu za Malawi na Zambia.

Kuanzishwa kwa Reli ya kusini itakuwa  ni ukombozi kwa mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara kwa kuwa mahitaji ya treni katika huduma ya usafiri na usafirishaji hivi sasa ni makubwa kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo uchimbaji wa makaa ya mawe mkoani Ruvuma.

Historia inaonesha kuwa Katika miaka ya 1950 Mkoani Lindi kulikuwa na reli inayotoka Nachingwea kupitia Mtama, Mnazi Mmoja, Mingoyo hadi Bandari ya Mtwara na ilikuwa ikisafirisha korosho, mbao, magogo na watu.

Naibu Waziri wa Uchukuzi amefanya ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ya kukagua mradi wa kiwanja cha Ndege cha Songea,mradi wa uboreshaji wa bandari ya Mbambabay na bandari 15 zilizopo katika ziwa Nyasa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.