SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 60 kuanza ujenzi barabara ya lami kilometa 60 kutoka Likuyufusi Kwenda Mkenda Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Barabara hiyo ni ya mpakani mwa Tanzania na Msumbiji yenye urefu wa kilometa 124 ambayo ina Kwenda hadi katika daraja la Mkenda Mto Ruvuma mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi amesema serikali kwa kuanzia inatekeleza mradi huo kwa kilometa 60 kuanzia Likuyufusi Manispaa ya Songea hadi Mkayukayu Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.