BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA)limetangaza rasmi kuanza kwa mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka 2024 huku jumla ya watahimiwa 557,731 wamesajiliwa kufanya mtihani huo ambao kati yao watahiniwa wa shule ni 529,321 na wakujitegemea ni 28,410.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA), Dk.Said Mohamed amesema mtihani huo unatarajiwa kufanyika Novemba 11 hadi Novemba 29 mwaka huu katika jumla ya shule za sekondari 5,585 na vituo vya kujitegemea 961.
Dkt .Mohamed amesema jumla ya watahiniwa wa shule walio na mahitaji maalumu ni 1,088 ambao kati yao 601 ni wenye uoni hafifu, 56 ni wasioona, 209 wenye ulemavu wa kusikia ,39 ni wenye ulemavu wa akili na 183 wenye ulemavu wa viungo vya mwili.
“Kati ya watahiniwa wa kujitegemea 28,410 waliosajiliwa, wavulana ni 11,167 sawa na asilimia 39.31 na wasichana ni 17,243 sawa na asilimia 60.69”
“Watahiniwa wa kujitegemea wenye mahitaji maalumu wako 18, kati yao wenye uoni hafifu ni mmoja na wasioona ni 16 huku wenye ulemavu wa viungo ni mmoja “amesema.
Vilevile amewataka wasimamizi wote walioteuliwa kusimamia upimaji kufanya kazi yao ya usimamizi kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.
Pia amesema wasimamizi hao wanapaswa kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanafanya upimaji wao ipasavyo ili wapate haki yao msingi ambazo ni pamoja na kupata mitihani yenye maandishi ya nukta nundu Kwa wanafunzi wasioona na maandishi yaliyokuzwa kwa wanafunzi wenye uoni hafifu.
Kwa upande wa wanafunzi amesema Baraza la mitihani halitarajii kuona mwanafunzi yoyote kujiusisha na vitendo vya udanganyifu na kutoa taadhari kuwa yoyote atakayebainika kufanya udanganyifu matokeo yake yatafutwa kwa mujibu wa kanuni za mitihani.
Sambamba na hayo amewataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mtihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyikaji wa upimaji huo.
Aidha amesema Baraza halitarajii kuona mwanafunzi yoyote anajiusisha na vitendo vya udanganyifu na kutoa taadhari kuwa yoyote atakayebainika kufanya udanganyifu matokeo yake yatafutwa kwa mujibu wa kanuni za mitihani.
Aidha amewataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mtihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyikaji wa upimaji huo.
Hata hivyo amesema baraza halitosita kukifuta matokeo kituo chochote cha mitihani endapo linajiridhisha pasipo shaka kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa upimaji wa kitaifa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.