• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

Imewekwa kuanzia tarehe: June 1st, 2025

Kwa macho ya kawaida, barabara ya lami ni njia tu ya kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine. Lakini kwa anayeipitia barabara ya Mbinga–Mbambabay mkoani Ruvuma , anajikuta akiingia katika sinema halisi ya mandhari ya kuvutia inayochorwa na milima,muonekano wa ziwa Nyasa na anga safi ya bluu. 

Barabara hii  yenye urefu wa  kilometa 66 iliyokamilika kwa kiwango cha lami nzito imegeuka kuwa kivutio cha kipekee cha utalii wa kuona mandhari (scenic tourism), ambapo kila kona inatoa fursa ya kupiga picha za kipekee, hasa pale inapojipinda katikati ya milima ya Livingstone huku ikielekea ziwani Nyasa mjini Mbambabay


Safari kuanzia Mbinga hadi Mbambabay sasa siyo tu njia ya kusafiri, bali ni tukio la kuvutia linalogusa hisia. Mandhari ya kijani kibichi, mashamba ya kahawa na kilimo cha ngolo yanayopamba milima, na upepo mwanana kutoka Ziwa Nyasa, huifanya safari hii kuwa tiba kwa akili na moyo. Wasafiri wengi, hasa watalii wa ndani na nje ya nchi, wameanza kuweka barabara hii kwenye orodha ya maeneo ya kutembelea kutokana na uzuri wake wa asili unaochanganyika na miundombinu bora ya kisasa.
Mbambabay, makao makuu ya ya Wilaya ya Nyasa, hapo awali kilikuwa  kijiji tulivu cha uvuvi, sasa inabadilika taratibu kuwa kituo cha utalii wa kimkakati. Hii ni kutokana na barabara hii mpya ambayo imefungua mlango wa uchumi na utalii kwa kuvutia wawekezaji na wageni. Hoteli ndogo ndogo, nyumba za wageni, na waendesha boti za kitalii kwenye Ziwa Nyasa wanaibuka, wakithibitisha kuwa lami si tu barabara bali ni daraja la maendeleo na urithi wa uzuri wa Mkoa wa  Ruvuma kuingia katika ramani ya ulimwengu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DKT Nchimbi awaongozawananchi kuuaga mwili wa Mzee Songambele

    June 02, 2025
  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.