Baraza la Wawakilishi wa Wazee wa Mila na Desturi mkoani Ruvuma limefanya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wapya, ambapo shughuli hiyo ilifanyika katika Makumbusho ya Majimaji, Manispaa ya Songea.
Uchaguzi huo ulihusisha makabila mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma, yakiwemo ya Wangoni, Wayao, Wanyasa, na Walendeule. Viongozi waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali ni pamoja na Willium Gama aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti, Salma Komba kuwa Makamu Mwenyekiti, Abasi Chitete kuwa Katibu Mkuu, na Ngaiwana Nkondora kuwa Katibu Msaidizi.
Katika uchaguzi huo pia, wajumbe wapya wa halmashauri kutoka wilaya mbalimbali walichaguliwa. Hawa ni pamoja na Sophia Namagono (Halmashauri ya Tunduru), Faustine Lehman (Mbinga), Tabia Kobe (Namtumbo), Abel Tawete (Madaba), Samuel Muhaiki (Nyasa), pamoja na Philip Shantembo na Jumanne Lukaba kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma, Anthony Luoga, aliwataka viongozi waliochaguliwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata misingi ya uongozi bora.
“Ninyi mnatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu ili wengine wawafuate. Msiwe viongozi wasiofaa kuigwa, bali onesheni heshima na uwajibikaji,” alisema Luoga.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Ruvuma, Suleimani Matata, aliwasihi viongozi hao kuendeleza mshikamano, kushirikiana kwa upendo, na kuepuka kuweka vikwazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya uongozi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.