• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BENKI ya NMB yatoa msaada wa vifaa vya milioni 32 mkoani Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: March 14th, 2021

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 32 katika wilaya za Namtumbo na Songea mkoani Ruvuma.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika hafla ya ujtoaji wa vifaa hivyo katika shule tatu za msingi zilizopo Manispaa ya Songea,Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Janeth Shango amezitaja shule zilizopata vifaa hivyo kuwa ni shule ya msingi Legele iliyopata mabati 60 kwa ajili ya kuezeka darasa la kwanza na choo.

Shule nyingine ni Mshanganokati iliyopewa madawati 80 na shule ya msingi Chandamali ambayo imepewa meza 21,viti 21 na kabati nne ambapo amesisitiza kuwa Benki ya NMB imeamua kushirikiana na jamii kwa kutoa msaada katika shule hizo tatu .

Katika Wilaya ya Songea Halmashauri ya Madaba,Meneja huyo wa Kanda amesema NMB  imetoa vitanda 25 katika shule ya sekondari Gumbiro,viti na meza 50 katika shule ya sekondari Nguluma vifaa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi.

Kwa mujibu wa Meneja huyo,Benki ya NMB katika wilaya ya Namtumbo imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Namtumbo vyenye thamani ya shilingi milioni kumi.

Shango amevitaja vifaa hivyo kuwa ni vitanda vitano vya wagonjwa na godoro zake,vitanda viwili vya kisasa vitakavyotumika wakati wa kujifungua akinamama na mashuka 25 kwa ajili ya vitanda hivyo.

“Kwa miaka kadhaa sasa NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi kwenye miradi ya elimu kwa kutoa madawati na vifaa vya kuezekea na kwenye afya kwa kutoa vitanda na magodoro yake’’,alisema.

Amesisitiza kuwa kupitia jamii,NMB inatambua kuwa wanapatikana wateja wake wengi,kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni wa Benki hiyo ambayo imezifikia wilaya zote nchini kwa asilimia 100.

Akizungumza katika hafla ya kugawa vifaa vya hospitali ya Namtumbo,mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo ambao amesema umeongeza vitanda  katika hospitali hiyo ambayo imeanza kulaza wagonjwa na kwamba kabla ya msaada huo hospitali  ilikuwa na vitanda kumi tu.

“Tuliamua kuanzia mwaka jana kuanza kulaza wagonjwa,hivyo tulianza na vitanda kumi,leo NMB wametuletea vifaa vya milioni kumi kwa ajili ya kusaidia hospitali yetu,tunawashukuru sana’’,alisisitiza Kizigo.

Kwa upande wake Meneja wa NMB Tawi la Songea David Zake akizungumza kwa nyakati tofauti katika zoezi la utoaji vifaa katika Manispaa ya Songea,amesema Benki ya NMB ni sikivu kwa sababu imekuwa inarudisha mapato yake ya asilimia moja kwa jamii kila mwaka .

Amesema hali hiyo ndiyo iliyosababisha shule tatu za msingi kuwa miongoni mwa shule ambazo zimepata mchango mkubwa kutoka NMB.

Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji  madawati hayo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro amesema NMB imekuwa karibu kwa jamii wilayani Songea kwa kutoa misaada mbalimbali katika shule na vituo vya afya ambapo amesema, Benki hiyo inaunga mkono jitihada za serikali kusaidia wananchi.

Naye Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Songea Zakia Fandey amesema msaada huo  utaongeza mahudhurio mazuri ya wanafunzi hasa katika shule msingi Mshanganokati iliyokuwa na uhaba mkubwa wa madawati na kwamba ufundishaji na ujifunzaji utaimarika .

Mkuu wa shule ya sekondari Gumbiro Jofrey Lyosi akizungumza baada yak kupokea msaada wa vitanda 25 kwa ajili ya kulala wanafunzi,amesema wanafunzi hao tangu mwaka 2012 wamekuwa wanalala chini kwenye magodoro bila kuwa na vitanda hivyo NMB ime,kuwa ukombozi kwa wanafunzi hao.

 Benki ya NMB katika nchi nzima ina matawi 225,mashine za kutolea fedha ATM zaidi ya 800,wakala zaidi ya 6,000 na idadi ya wateja zaidi ya milioni tatu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Machi 14,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.