BENKI ya NMB imeto msaada wa vitanda 80 vyenye thamani ya shilingi milioni 20 katika shule mbili za Halmashauri ya Songea vijini Mkoani Ruvuma
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini Janeth Shango amezitaja shule ambazo zimepata msaada huo na kumkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma Menejimenti na Utawala Bora Jenista Mhagama.
Shango amezitaja hizo shule ya sekondari ya Jenista Mhagama iliyopata vitanda 40 pamoaja Shule ya sekondari ya kilagano nayo imepata vitanda 40.
Akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais menejimenti na Utawala Mh. Jenista Mhagama baada ya kukabidhi msaada huo wenye thamani ya milioni 20 katika sekondari zote mbili amesema Benki ya NMB wapotayari kusaidia katika maswala ya Elimu pamoja na Afya.
“Vitanda hivi ambavyo tunavikabidhi leo,ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzani tunao wajibu wa kuhakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayopata’’,amesema Shango.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, Waziri Jenista Mhagama ameipongeza NMB kwa kutoa msaada huo wa vitanda kwa shule mbili za Halmashauri Wilaya Songea vijijini ambapo amesema msaada huo utasaidia kuboresha taaluma kwa wanafunzi.
“Nipende kuwashukuru kwa dhati benki ya NMB kwa msaada huu wa vitanda 80 katika shule hizi na imekuwa ikijitoa kwa jamii na leo tumeshuhudia imetoa msaada huu kwa lengo la kutatua changamoto za maradhi kwa wanafunzi wetu tuwahakikishie sisi kama Serikali tutashirikiana nanyi bega kwa bega ”
Benki ya NMB imekuwa kila mwaka inatoa misaada mbalimbali katika shule za Mkoa wa Ruvuma ambapo mwezi uliopita ilisaidia vifaa vya thamani ya milioni 15 kwenye shule tatu katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.