Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na kushamiri kwa Biashara ya makaa ya mawe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara yake kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema katika ziara yake ametembelea mgodi mmoja tu wa Kampuni ya JITEGEMEE katika kijiji cha Ntunduwaro Kata ya Ruanda Halmashauri ya Mbinga ambapo mgodi huo pekee umetoa ajira za kudumu 85 na vibarua 150 ambao wanalipwa kwa siku 15,000 kila mmoja.
Amesema hiyo ni faida kubwa kwa serikali na wananchi kwa kuwa kuna idadi kubwa ya madereva na utingo ambao wanahudumiwa na mamalishe kwenye eneo hilo ambao wananufaika.
Katika Mkoa wa Ruvuma kuna Kampuni 14 za uchimbaji wa makaa ya mawe ambazo zinalipa kodi na tozo mbalimbali serikalini sanjari na kutoa ajira
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.