Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,vyoo na ukamilishaji wa ujenzi wa maabara katika shule za sekondari na Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Afisa mipango wa Halmashauri hiyo Nyange Athuman amesema fedha hizo tayari zimeingizwa kwenye akaunti za shule husika kwa ajili ya kazi ya ujenzi na ukamilishaji wa miradi iliyokusudiwa kutekelezwa kwenye shule hizo.
Nyange ametoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha hizo kuwa ni milioni 210 zitatumika kukamilisha ukarabati wa maabara katika shule za sekondari saba ambazo kila shule zimepata mgao wa shilingi milioni 30, shilingi milioni 266,400,000 zitatumika kujenga vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za msingi na sekondari.
Amesema kati ya fedha hizo shilingi milioni 820 zitatumika kuendeleza ujenzi wa sekondari mpya ya wasichana ya Jenista inayojengwa katika Kata ya Parangu Kijiji cha Parangu
Ameongeza kwakusema kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa shule tatu za sekondari zimebahatika kupata mgao ambapo shule ya Sekondari Nalima na Namihoro zimepata milioni 53,200 000 kila moja na shule ya sekondari Muhukuru imepata milioni 40.
Adha kwa upande wa ujenzi wa matundu vyoo sekondari ya Nalima na Namihoro zimepata shilingi milioni 13,200,000 kwa kila shule.
Amezitaja Shule za msingi ambazo zimepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarsa kuwa ni Magagura,Matama,Matimira, Mbinga mhalule ambapo kila shule imepata mgawo wa shilingi milioni 13,200,000.
Amesema shule za msingi Putire,Kilagano,Kizuka,Matimira na Mbinga mhalule zimepata fedha toka Serikali kuu za EP4 kwa ajilii ya ujenzi wa matundu sita ya vyoo kwa kila moja na vyumba viwili vya madarasa kwa kila shule.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri hiyo Bumi Kasege amezitaja shule saba kati ya 16 za Serikali zilizo pewa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara kuwa ni shule ya Sekondari Namihoro, Darajambili, Lupunga,Matimira,Muhukuru,Muhukuru barabarani na Liganga ambapo kila shule imepata shilingi milioni 30.
Kasege amesema ukarabati wa kukamilisha maabara hizo umeanza tangu juni mosi mwaka huu na unatarajia kukamilika ifikapo juni 30 mwaka huu kulinga na miongozo na makubaliano ya fundi kiongozi aliyepata dhamana ya kazi hiyo
“Nimefuatilia kazi hiyo kwakufika kwenye shule hizo na kubaini hali ya ujenzi inanyoenda vizuri hadi juni 30 na tegemea kazi itakuwa imekamikika”, alisisitiza kasege.
Akizungumza kwaniaba ya mafundi viongozi Tito Mwenda ambaye anakamilisha ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari Muhukuru amesema wanauhakika wa kukamilisha kazi kwa wakati kwasababu hakuna changamoto itakayokwamisha na vifaa vyote vinavyo hitajika vimenunuliwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma inajumla ya shule za Sekondari 21 kati ya hizo 16 ni za Serikali na zinazo milikiwa na watu binafsi ni tano,shule za Msingi ni 75 za Serikali ni 73 na zinazomilikiwa watu binafsi ni mbili.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari Songea DC
14 /06/2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.