• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BILIONI 145 kumaliza kero ya maji mjini Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: September 18th, 2024

WIZARA  ya maji,imepanga kutumia kiasi cha  Sh.bilioni 145.77 ili  kujenga mradi  wa maji wa miji 28 ambao utaongeza  upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Hayo yamesemwa  na Waziri wa maji Jumaa Aweso, baada ya kukagua ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi takribani lita milioni mbili linalojengwa katika mtaa wa Mahenge kata ya Mjini Manispaa ya Songea.

Waziri Aweso,amewapongeza watumishi wa wizara ya maji wakiwemo wa  mkoa wa Ruvuma kwa kazi nzuri ya kutatua kero pamoja kuboresha huduma ya maji  safi na salama katika maeneo mbalimbali.

Alisema,siku za nyuma mkoa wa Ruvuma ulikuwa kama kichaka kwa watendaji kula fedha zinazoletwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji,na kutolea mfano mradi wa maji Litola-Kumbara ambao ulisimama zaidi ya miaka 12 bila kukamilika wakati Serikali ilishatoa fedha  ili kukamilisha ujenzi wake.

“Tangu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani ameleta mapinduzi makubwa kuhusu huduma ya maji kwani sasa miradi mingi ya imetekelezwa na wananchi wanapata maji kwenye maeneo yao,haya  ni mafanikio makubwa kwetu sisi kama Serikali”alisema Aweso.

Aidha alisema,katika mkoa wa Ruvuma kuna miradi zaidi ya 30 inayoendelea kutekelezwa  na itakapokamilika itafikisha malengo ya  Serikali ya kufikisha asilimia 95 mijini na asilimia 85 vijijini ifikapo mwaka 2030.

Alitaja baadhi ya miradi  hiyo ni mradi wa maji  wa Mtyangimbole uliopo katika Halmashauri ya  wilaya Madaba,mradi wa maji Misechela wilaya ya Tunduru na mradi wa maji Liuli uliopo wilaya ya Nyasa.

Waziri Aweso,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa magari ya kuchimba visima kwenye mikoa yote yenye changamoto kubwa ya upatikaji maji wa maji,vifaa vya utafiti vya maji na kuchimba mabwawa kwenye maeneo yasiyokuwa na vyanzo vya uhakika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka  ya maji safi na usafi wa mazingira katika  Manispaa ya Songea(Souwasa)Mhandisi Patrick Kibasa alisema,mradi ulianza kutekelezwa mwezi Januari 2024 na mpaka kufikia  mwezi Julai utekelezaji wake umefikia asilimia 3.9.

Kibasa alisema,Serikali imemlipa mkandarasi fedha za awali Sh.bilioni 21,865,952,341.45 sawa na asilimia 15 kati ya Sh.bilioni 154,773,015,609.69 ambazo ziko kwenye mkataba wa ujenzi.

Kibasa alitaja kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni ujenzi wa miundombinu ya kudaka maji katika mto Njuga uliopo kijiji cha Kikunja katika Halmashauri ya wilaya Songea ili kuzalisha maji lita milioni 16.5 kwa siku.

Alitaja kazi nyingine zilizopangwa kutekelezwa katika mradi huo ni ujenzi wa matenki matatu ya kuhifadhi maji yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 9,kujenga miundombinu ya mabomba ya kusafirisha maji kilometa 30.2 na kujenga miundombinuya bomba za usambazaji maji km 34.1.

Aliongeza kuwa,mradi huo ukikamilika utaongeza upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea kwa zaidi ya asilimia 95,hivyo kutosheleza mahaitaji ya maji safi na salama kwa wakazi wa Manispaa hiyo.

Alieleza kuwa,katika utekelezaji wa mardi huo changamoto kubwa ni mabadiliko ya chanzo cha maji kutoka bwawa ambalo awali lilionyesha kuwa na kiwango kikubwa cha cha maji yanayohitajika kwenda kwenye  mto,lakini sasa yamepungua  na  kuchelewesha utekelezaji wa mradi.

Alisema baada ya mabadiliko hayo  kwenye chanzo cha maji,mkandarasi amewasilisha upya gharama za ujenzi wa ambazo zinazidi  gharama awali ambazo ni Sh.bilioni 145,773,015,609.69.
Kibasa alieleza kuwa, chanzo cha maji kimegharimu Sh.bilioni 58.6 wakati  ujenzi wa bwawa umegharimu Sh.bilioni 62.5 na ujenzi wa mtambo wa kuchuja  na kutibu maji gharama ni Sh.bilioni 48.8 wakati gharama za awali kama ilivyo kwenye mkataba ilikuwa Sh.bilioni 22.6.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas alisema,mradi  wa  maji wa miji 28 utakapokamilika utakuwa na mafanikio makubwa kwa kuboresha upatikanaji wa  maji safi na  salama kwa wakazi wa Manispaa ya Songea.

Rc Abbas,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,kwa kutoa zaidi ya Sh.bilioni 3 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji katika manispaa ya Songea na Sh.bilioni 20.1 kwa ajili ya miradi ya maji inayotekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa).

Naye Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt Daamas Ndumbaro alisema,huduma ya maji inaendelea vizuri,lakini changamoto kubwa ni kukua kwa mji wa Songea na ongezeko kubwa la watu wanaohitaji huduma ya maji kwa  matumizi mbalimbali.

Dkt Ndumbaro alisema,kwa sasa mahitaji ya maji katika manispaa ya Songea ni lita milioni 21,278,000 wakati uzalishaji wa maji kwa sasa ni lita milioni 12,030,000.

Alieleza kuwa,mradi huo ukikamilika utaongeza upatikanaji wa maji hadi kufikia lita milioni 27 ambazo zitatosheleza kwa mahitaji ya wakazi wa mji huo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.