• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BILIONI 22 kufanyia matengenezo barabara za Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: August 6th, 2024

WAKALA wa barabara za mijini na vijijini(TARURA) Mkoa  wa Ruvuma,kwa mwaka wa fedha 2024/2025 umeidhinishiwa katumia kiasi cha Sh.bilioni 22,194,409,504.77 kwa ajili ya kufanya matenengezo ya barabara zake.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Silvester Chinengo  amesema ,kati ya fedha hizo kutoka  Mfuko Mkuu wa Barabara  ni Sh.bilioni 7,894,961,998.36 na mfuko mkuu wa  serikali wa kila jimbo shilingi shilingi bilioni 4,500,000,000.00 ,fedha za tozo ya mafuta Sh.100 kwa lita ni Shilingi bilioni 9,799,447,506.41.

Chinengo amesema hayo   kwenye hafla fupi ya utiaji saini mikataba ya matengenezo ya Barabara iliyoshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed mjini Songea.

“mpaka sasa TARURA tumekamilisha manunuzi ya miradi 50  yenye gharama ya Sh.bilioni 14,19,607,702.00 ambapo jumla ya kilometa 1,079 za barabara zitafanyiwa matengenezo ya aina mbalimbali pamoja na ujenzi wa makalavati na madaraja”alisema Chinengo.

Kwa upande wake Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema ,serikali kupitia TARURA itahakikisha inawalipa Wakandarasi fedha zao ili kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ameziagiza Taasisi za serikali mkoani humo,kulipa madeni  ya wakandarasi kwa wakati  ili kuwaepusha wakandarasi kuingia kwenye migogoro mbalimbali ikiwemo kunyang'anywa na  kuuziwa  mali zao na taasisi za fedha kutokana na fedha walizokopa kama mitaji katika shughuli zao.

Amesisitiza kuwa ,serikali kupitia sekta ya mawasiliano ya barabara imejipanga kuona sekta ya barabara inaimarika ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa mazao kutoka shambani kwenda mijini kwa ajili ya kupata soko la uhakika.

Katika hatua nyingine Kanali Abbas,amezitaka Taasisi za Serikali mkoani humo, kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa na kutoa upendeleo  kwa wanawake wanaofanya kazi za ukandarasi ili kuwajengea uwezo na kunufaika na fedha zinazotolewa

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo,amewataka watendaji wa TARURA kuwafuatilia kwa karibu wakandarasi ili miradi inayotekelezwa ikamilike kwa muda uliopangwa na kwa viwango vinavyohitajika.


Naye Mkuu wa  TAKUKURU  mkoani Ruvuma Hamza Mwenda amesema , TAKUKURU itahakikisha inafuatilia miradi yote iliyopangwa kutekelezwa ili kujiridhisha ubora wa miradi husika.

Mwakilishi wa Wakandarasi wa Mkoa wa Ruvuma Vales Urio kutoka Kampuni ya  Ovans Contructions Ltd,ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwaamini na kuwapa kazi za ujenzi wa miradi ya barabara na kuhaidi watekeleza miradi hiyo kwa ubora ili kuleta tija kwa mkoa na Taifa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.