Bilioni 23.4 zajenga vihenge vya kisasa vya kuhifadhia mahindi mkoani Ruvuma
Imewekwa kuanzia tarehe: August 11th, 2020
Serikali ya awamu ya tano inatekeleza mradi wa Ujenzi wa vihenge 12 na maghala 2 ya kuhifadhia nafaka katika eneo la Ruhuwiko Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ameuletea Mkoa wa Ruvuma shilingi Bilioni 23.4 kwa ajili ya ujenzi wa vihenge 12 na maghala mawili ya kuhifadhia nafaka yaliyopo katika Manispaa ya Songea. na kwamba mradi wa Ujenzi wa maghala hayo bado unaendelea.