• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BILIONI 33 ZANUFAISHA KAYA MASIKINI RUVUMA

Imewekwa kuanzia tarehe: July 20th, 2023

SERIKALI imetoa zaidi ya shilingi bilioni 33 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kunusuru kaya kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mkoani Ruvuma.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa TASAF katika kipindi cha pili kwenye mkutano wa mwaka 2022/2023 uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea,mratibu wa TASAF Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira amesema serikali ilitoa kiasi hicho cha fedha katika Halmashauri zote kuanzia Julai 2020 hadi Juni 2023.

Hata hivyo amesema kati ya fedha hizo zaidi shilingi ya bilioni 30 zilitolewa kwa walengwa,shilingi bilioni 1.8 zilitumika kwa ajili ya ufuatiliaji  ngazi ya Halmashauri na shilingi milioni 295.22 zilitumika kwa ajili ya ufuatiliaji ngazi ya vijiji.

“Lengo la mpango wa TASAF ni kuziwezesha kaya maskini sana kuongeza kipato,fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu,Mkoa wa Ruvuma unatekeleza mpango huu ambao ulianza kutekelezwa katika Halmashauri ya Tunduru mwaka 2013’’,alisema Mlimira.

Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya ajira za muda kwa kaya masikini,Mratibu huyo wa TASAF amesema mradi huo umelenga kutoa ajira kwa kaya masikini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa kushiriki katika kutekeleza miradi mbalimbali inayoibuliwa na jamii na kulipwa ujira.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa visima vya asili,utengenezaji Barabara,ujenzi wa vivuko ambapo katika Mkoa wa Ruvuma hadi sasa miradi 663 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni nne imetekelezwa katika vijiji 649.

Akizungumza wakati anafungua mkutano huo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas  amesema kikao hicho kimelenga kuwajengea uelewa wa sehemu ya pili ya mpango wa kunusuru kaya masikini kwa viongozi ngazi ya Mkoa na wilaya.

Amesema Halmashauri zote zinatekeleza mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo hadi kufikia Juni 2023 Mkoa ulikuwa na kaya 65,089 za walengwa zinazoendelea kunufaika na utekelezaji wa TASAF ambao upo katika sehemu ya pili ya utekelezaji.

Amesema mpango huo umekusudia kuongeza kipato,kuongeza rasilimali za lishe,kuongeza vitegauchumi na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya,maji na elimu.

Amesema serikali kwa kushirikiana na wadau imewekeza fedha za kutosha katika utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini ambapo ameagiza Halmashauri zote kuhakikisha kuwa fedha hizo zinasimamiwa kikamilifu ili kuhakikisha zinaleta tija kwa jamii.

Amewaagiza wadau wote mkoani Ruvuma kutoa elimu kwa walengwa ili wafuzu kutoka katika kaya masikini na  kaya nyingine masikini ambazo hazikuwa kwenye mpango huu ili ziweze kupata nafasi.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa kunusuru kaya masikini na kuwezesha kutekeleza miradi mingi ya TASAF.

Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma  zinatekeleza mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBUNGE Kawawa aleta neema Namtumbo

    May 11, 2025
  • KIONGOZI Mwenge wa uhuru ashiriki upandaji miti Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru waweka jiwe la msingi shule ya amali Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru wazindua jengo la EMD Peramiho

    May 10, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.