Serikali ya Awamu ya sita imetoa zaidi ya shilingi bilioni 34 kuboresha sekta ya elimu mkoani Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema fedha hizo zimetumika kuboresha mazingira ya kufundishia na ya kujifunzia kwa kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu kwa lengo la kuhakikisha watoto wanapata elimu katika mazingira bora na yenye staha,
Amesema Fedha hizo zimetumika katika ujenzi wa mabweni 35, matundu ya vyoo 1444, vyumba vya madarasa 301,nyumba za walimu tisa na vichomea taka 12.
Ameongeza kuwa fedha hizo pia zimetumika kujenga shule mpya 21 za sekondari ,majengo ya utawala 12 na vituo vya walimu 12.
Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma kwa kipindi cha miaka mitatu umepokea walimu wa ajira mpya 877 ambapo kati yao walimu wa shule za msingi walikuwa 489 na sekondari 388
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.