Barabara mpya inayounganisha vijiji mbalimbali na mji wa Tunduru ikiwa ni jitihada za wakala wa Barabara za vijijini na mijini Tarura kuufikisha mawasiliano katika maeneo yote.
WAKALA wa Barabara za vijijini na mijini(TARURA)mkoa wa Ruvuma,katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,umepokea jumla ya Sh. bilioni 43,924,114,171.33 kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Tarura mkoani Ruvuma Wahabu Nyamzungu,wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miundombinu ya Barabara zinazosimamiwa na Tarura katika kipindi cha miaka miwili ofisini kwake mjini Songea.
Nyamzungu alisema, fedha hizo zimeiwezesha Tarura kufanya matengenezo ya barabara kwa kiwango cha changarawe urefu wa kilomita 482.132,ujenzi wa barabara za lami kilomita 25.053,ujenzi wa madaraja 40 na ujenzi wa mifereji mita 3,400.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.