SERIKALI ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia S. Hassan imetoa bilioni 7 kwa lengo la kuboresha utoaji huduma ya Afya kwa Wananchi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma
Akizungumza mbele ya Wataalamu kutoka Hospitali ya kanda ya Mbeya Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea. Dr, Magafu Majura amesema Hospitali imepokea Shilingi bilioni 7 kukamilisha mipamgo mikakati ya utoaji huduma kwa wananchi.
Dr. Majura amesema fedha hizo zimeelekezwa katika kujenga jengo la wagonjwa wa nje, jengo la huduma ya mionzi pamoja na nyumba moja ya mtumishi pia na ukarabati wa jengo la wangonjwa wenye uangalizi maalumu na jengo la dawa
Mbali na ujenzi na ukarabati huo ameeleza kuwa Serikali imeamua kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi kwani imenunua vifaa tiba kimoja wapo ni Mashine ya uchunguzi ya CT-Scan ambayo itahudumia na kutoa matibabu kwa haraka na itasidia kuondoa msongamano wa wangonjwa
“Hii itatusaidia kwa wagongwa watakao hitaji kutibiwa katika Hospitali zetu za kanda na taifa kuweza kuanza kupata matibabu wakiwa bado wapo hapa kwamaana ya kuwasiliama kupitia tiba mtandao na madaktari wabobezi waliopo katika Hospitali zetu kubwa na kutupa majibu” Amesema Dr. Majura
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya kanda ya Mbeya Dkt. Godlove Mwanji amesema Serikali imeamua kuboreha huduma za Afya ili wananchi wawe na uhakika wa kupata matibabu na kuepukana na gharama za kufuta matibabu kwenye hospitali kubwa za kitaifa
“Furaha yetu ni kwamba tumekuta miradi yoye hii imefikia hatua nzuri na siku si nyingi tutarajie kuwa itaanza kuwahudumia Wananchi tumeona vifaa vya kisasa vikitumika kutoa huduma jambo hili ni lakupongeza na kutoa shukrani kwa Serikali”amesema Dkt. Mwanji
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharula na ajali Dr. Edson Francis ameeleza hali ilivyo sasa baada ya kukamilika kwa jengo hilo la wagonjwa wa dharula ambapo limesaidi kuhudumia wa wagonjwa wengi kwa haraka na kupata matibabu kwa muda mfupi
Hata hivyo Serikali imeboresha upatikanaji huduma mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma kwa nunua mashine ya uchunguzi ya CT-Scan kwa mara ya kwanza ambayo itasaidia Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kutosafiri umbali mrefu Mbeya, Dodoma na Dar es salaamkwaajili ya vipimo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.