• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BILIONI 81 za Rais Samia zilivyoanza kujenga bandari ya kisasa Mbambabay

Imewekwa kuanzia tarehe: June 4th, 2024

 SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 81  kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi wa bandari ya Mbambabay ziwa Nyasa mkoani Ruvuma.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mhandisi wa Mamlaka ya  Bandari  Tanzania (TPA) Mhandisi Fabian Paul wakati anatoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bandari ya Mbambabay kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed  ambaye amefanya ukaguzi wa eneo la ujenzi wa mradi huo mjini Mbambabay.

Mhandisi Paul amesema TPA Desemba 2023 iliingia mkataba wa miezi 24  na Kampuni ya M/S Xiamen Ongoing Constructio Group ya nchini China kwa ajili  kuanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa bandari ya Mbambabay.

Amesema mradi wa ujenzi wa bandari hiyo mpya unatarajia kukamilika Januari 26,2026 ambapo amezitaja kazi zinazofanyika kuwa ni usanifu,ujenzi wa gati lenye uwezo wa kuegesha meli mbili zenye uzito wa tani 5,000 na ujenzi wa jengo la utawala.

Mhandisi Paul ameyataja majengo mengine kuwa ni ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari,ujenzi wa jengo la abiria,ghala na karakana,ujenzi wa barabara za ndani na mzunguko,kuchimba kwa ajili ya kuongeza kina cha maji eneo la kupaki na maingilio ya meli,kuweka mifumo ya umeme,maji,ulinzi,ujenzi wa uzio na kujenga eneo la sakafu ngumu lenye ukubwa wa mita za mraba 20,000 kwa ajili ya kuhudumia shehena.

 Hata hivyo amesema utekelezaji wa mradi huo hadi sasa umefikia asilimia 35 katika ukusanyaji wa vifaa na mitambo ya ujenzi,ujenzi wa ofisi kwa ajili ya mradi  umefikia asilimia 75,kazi ya usanifu wa kina imefikia asilimia 25 na kazi ya kutoa mawe eneo la ujenzi imefikia asilimia 20.

“TPA inatoa shukurani za dhati kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha taslimu shilingi bilioni 81 kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi huu mkubwa katika ziwa Nyasa’’,alisema.

Ameutaja mradi huo ukikamilika,makao makuu ya bandari za Ziwa Nyasa yanatarajia kuhama kutoka Kyela mkoani Mbeya na kuhamia Mbambabay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.

Akizungumza baada ya kukagua eneo la mradi wa bandari ya Mbambabay,Mkuu wa Mkoa  wa Ruvuma Kanalii Ahmed Abbas Ahmed  amesema kukamilika kwa bandari hiyo kutaongeza ukuaji wa uchumi wa Taifa na Mkoa na kwamba mradi huo pia utatengeneza ajira kwa vijana.

Amesisitiza kuwa bandari ya Mbambabay itaiunganisha Tanzania na mataifa mengine ya  Msumbiji na Malawi hivyo kuimarisha Zaidi mahusiano na mataifa hayo na kukuza uchumi.

Mkuu wa Mkoa ameiagiza TPA kulipa haraka fidia za barabara,makaburi na fidia zingine ili wananchi waweze kupisha utekelezaji wa mradi na kwamba wahakikishe wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika hatua za utekelezaji wa mradi huo ili waone mradi ni wao.

“Zile kazi ambazo si za kitaalam sana tuwape wananchi wetu wa maeneo haya,lakini hata zile kazi za kitaalam ambazo watu wetu wanaweza  kufanya wapewe kipaumbe wao kwanza kabla ya kutoka nje ya Mkoa’’,alisisitiza.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameipongeza Kampuni inayotekeleza mradi huo kwa kuwa na vifaa muhimu ambapo ameagiza kuongeza vifaa Zaidi na nguvu kazi ili kutekeleza mradi huo ndani ya mkataba.

Amesisitiza kuwa atafuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo kwa sababu mradi huo unachukua sura ya kimataifa na kiuchumi ambapo mradi unaweza kusaidia kukuza uchumi na kuongeza mapato.

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.