Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhandisi Maua Mgallah amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024 wamepanga kutumiza zaidi ya Sh.bilioni 5.47 kwa ajili ya kutekeleza miradi sita mipya ya maji.
Mgallah ametaja baadhi ya miradi hiyo ambayo imeanza kutekelezwa ni mradi wa maji Tuwemacho utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni moja na mradi wa maji Msinji unaotekelezwa kwa zaidi ya shilingi bilioni moja.
Miradi mingine ni Hulia unaotekelezwa kwa Sh.bilioni 1,2,mradi wa maji Namwinyu wenye thamani ya Sh.milioni 450 na mradi wa maji Nakapanya ambao umetengewa jumla ya Sh.milioni 150.
Hata hivyo amesema ,miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na itakapokamilika itaongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 7.2 hivyo kufikisha asilimia 89.8 katika maeneo ya vijijini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.