Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya maboresho makubwa ya huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza kwenye ufunguzi na uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya hospitali hiyo mjini Songea Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Songea Dr.Magafu Majura amesema Katika kipindi cha 2020-2024, serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 8.6 kwa ujenzi wa majengo na ununuzi wa vifaa tiba.
Ameitaja Miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kuwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje,OPD, wodi ya wagonjwa wa dharura , na jengo la mionzi ambalo limeanza kutumika.
“Maboresho ya hospitali yameongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa kiasi kikubwa,Changamoto kuu zinazoikabili hospitali ni pamoja na upungufu wa watumishi kwa asilimia 25,Ukosefu wa baadhi ya dawa ,vifaa tiba na Miundombinu dhaifu katika baadhi ya maeneo”,alisema Majura.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed aliyewakilishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano amesema lBodi mpya imepewa jukumu la kusimamia huduma bora kwa wananchi, kuimarisha uwajibikaji wa watendaji, na kushughulikia changamoto zilizopo. Hata hivyo amesema Serikali itaendelea kutoa msaada wa rasilimali, mafunzo, na miongozo ili kuhakikisha mafanikio ya bodi.
Ametoa rai kwa Mwenyekiti wa Bodi mpya pamoja na wajumbe kuhakikisha mipango ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu.
Bodi mpya ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, iliyozinduliwa rasmi,iliundwa Oktoba 8, 2024, unatarajia kumaliza muda wake Septemba 4, 2027.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.