Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kwa namna ya pekee anamshukuru Rais Dkt. John Magufuli kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya uboreshaji wa kiwanja cha ndege wa Songea ambapo ndege kubwa za abiria zitaanza kutua na kuufanya Mkoa wa Ruvuma sasa kufunguka katika usafiri wa angani.
Anasema Rais ameupatia Mkoa wa Ruvuma shilingi bilioni 37.09 kwa ajili ya upanuzi wa kiwanja cha ndege Songea kwa kiwango cha lami na kwamba kiwanjahicho sasa kina urefu wa kilomita 1.74 na upana mita 30 na kwamba Ujenzi umefikia zaidi ya asilimia 60 ya utekelezaji na kuwezesha ndege aina ya bombardier kuruhusiwa kutua.
Mndeme anasisitiza kuwa Kukamilika kwa kiwanja hicho kutafungua anga la mkoa wa Ruvuma na kuruhusu wawekezaji na watalii kufika Ruvuma kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji na utalii hivyo kuchangia pato la taifa na kuinua uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
“Ahsante Rais Magufuli kwa utekelezaji wa miradi hii kwa vitendo ambayo imewaingiza wananchi wa mkoa wa Ruvuma katika uchumi wa kati kwa kasi, sasa Ruvuma itaonekana Angani,Majini na Barabarani ’’anasema Mndeme.
Serikali imesema ndege aina ya Bombardier Q400 itaanza tena safari zake za kuruka na kutua katika Kiwanja cha Ndege cha Songea Septemba mwaka huu ili kufungua fursa za mbalimbali za kiuchumi,kijamii na kitalii mkoani Ruvuma.
Kiwanja cha ndege wa Songea ni miongoni mwa viwanja bora vya ndege Tanzania ambacho kilijengwa kati ya mwaka 1974 hadi 1980 na kiliwekewa lami hivyo kuwa na uwezo wa kutua ndege majira yote masika na kiangazi.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.