Katika kuendeleza kauli mbiu yao ya “Tupo Karibu Yako”, Benki ya NMB kupitia tawi lake la Namtumbo imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuijali jamii kwa vitendo—safari hii kwa kugusa sekta ya elimu wilayani Namtumbo.
.Kupitia mchango wa madawati 150 yenye thamani ya shilingi milioni 14.25, NMB imezinufaisha shule tatu: Pamoja High School, Nanungu Secondary, na Selous Primary School. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika rasmi katika shule ya msingi Selous na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya, aliyekuwa mgeni rasmi.
Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Olipa Hebel amesema Kwa muda mrefu sasa, Benki ya NMB imeendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo nchini, hasa katika kuinua mazingira ya elimu kwa kutoa misaada inayogusa moja kwa moja ustawi wa wanafunzi na walimu.
Mchango huu ni ushahidi wa wazi kuwa benki hiyo haiko tu kwa ajili ya huduma za kifedha bali pia inashiriki kikamilifu katika kujenga kesho bora kwa watoto
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.