• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BOMBARDIER kutua Songea Septemba 2020

Imewekwa kuanzia tarehe: August 9th, 2020

BOMBARDIER KUTUA SONGEA SEPTEMBA

Serikali imesema ndege aina ya Bombardier Q400 itaanza safari zake za kuruka na kutua katika Kiwanja cha Ndege cha Songea ifikapo mwezi Septemba mwaka 2020 ili kufungua fursa za kiuchumi na kijamii.

Amezungumza hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akiwa mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya kukagua hali ya miundombinu ya barabara, madaraja na kiwanja cha ndege ambapo ameridhishwa na hatua zilizofikiwa za ukarabati wa kiwanja hicho ikiwemo uboreshaji wa barabara ya kutua na kuruka ndege yenye urefu wa mita 1740, eneo la maegesho ya ndege na taa za kuongozea ndege.

"Hadi sasa hatua zilizofikiwa ni nzuri na kufikia mwisho wa mwezi huu wa nane mkandarasi atakuwa amekamilisha kujenga mita 1200 za barabara ya kuruka na kutua ndege ambayo itaweza kuruhusu ndege kubwa aina ya Bombardier kuanza kutua", amesema Waziri Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe amesema kuwa kazi yote ya ukarabati na uboreshaji wa kiwanja hicho unagharamiwa na fedha za ndani kwa kiasi cha shilingi bilioni 37 na unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2020.

Aidha, ameongeza kuwa kukamilika kwa kiwanja hicho kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo katika ukanda huo ambao awali ulikuwa na changamoto kubwa ya usafiri wa anga.

"Ujio wa ndege hizi utapunguza gharama za usafiri wa ndege ambapo awali gharama ilikuwa fedha za kitanzania zaidi ya shilingi laki tano kwa safari moja na hii kupelekea watu wachache kumudu gharama hizo", amesisitiza Waziri Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe ameeleza azma ya Serikali ni kuendelea na uboreshaji na ukarabati wa viwanja vingine 10 hapa nchini kwa lengo la kuinua na kukuza uchumi wa Taifa.

Awali akitoa taarifa ya mradi, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Ruvuma Mhandisi Lazeck Alinanuswe, amemueleza Waziri huyo kuwa mpaka sasa mkandarasi amefikia asilimia 60 ya kazi ya ujenzi wa tabaka jipya la lami katika Kiwanja hicho.

Mhandisi Alinanuswe, amefafanua kuwa uboreshaji na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Songea unatekelezwa na Kampuni ya CHICO na kusimamiwa na Kampuni ya Atkins J/V Advance Engineering kwa muda wa miezi 20.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.