Akitoa taarifa ya Bonde la Maji la ziwa Nyasa Mkurugenzi wa Bodi Bonde la Maji la Ziwa Nyasa Mhandisi Arice Engalabeth BONDE la Maji la Ziwa Nyasa lina uwezo wa kutumia maji milimita za ujazo zaidi ya milioni 12 kwa mwaka.
Mhandisi Engalabeth amesema kati ya milimita hizo za maji,meta za ujazo milioni 107 ni za maji chini ya ardhi na kwamba bonde la maji la ziwa Nyasa ni bonde la pili kwa wingi wa maji ya juu ya ardhi kati ya mabonde ya maji tisa yaliyopo nchini.
Hata hivyo amesema bonde la maji la ziwa Nyasa ni la mwisho kwa wingi wa maji chini ya ardhi kati ya mabonde tisa yaliyopo nchini na kwamba bonde hilo lina vituo 54 vya kufuatilia mwenendo wa maji ambapo katika Mkoa wa Ruvuma vituo hivyo vipo katika mito ya Ruhuhu,Ngaka,Lutukira na Lumecha na katika ziwa Nyasa kuna vituo vitatu vinavyofuatilia wingi wa maji kwa usawa wa ziwa.
“Katika Mkoa wa Ruvuma tumeunda Jumuiya sita za watumiaji maji,Mkoa wa Ruvuma una mito mingi ambayo inatiririsha maji,hivyo tunawajibu wa kuhakikisha tunatunza vyanzo vya maji ili viweze kutusaidia kwa maendeleo ya kiuchumi kwa kizazi cha sasa na kijacho’’,alisisitiza Mhandisi Arice.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.