Benki ya Tanzania (BoT) tawi la Mtwara imefanya semina ya uwekezaji wa dhamana katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Semina hii ililenga kuwajengea uelewa wananchi kuhusu fursa za uwekezaji kwenye dhamana za serikali, utaratibu wa minada ya dhamana za serikali pamoja na faida zake.
Semina hiyo iliwezeshwa na wataalamu kutoka Benki ya Tanzania, ambao walitoa maelezo ya kina kuhusu aina mbalimbali za dhamana zinazopatikana, faida za kuwekeza kwenye dhamana, na jinsi ya kushiriki katika uwekezaji huo.
Pia, wataalam wa BOT walisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa semina hiyo, Ndg. David Mponeja, Meneja wa Fedha na Utawala wa BoT tawi la Mtwara, alieleza kuwa wananchi wanapaswa kufahamu jinsi ya kutunza fedha na kutumia taasisi za fedha kwa njia sahihi ili kutekeleza sera ya fedha kwa ufanisi.
Semina hii ni hatua muhimu katika kuwajengea wananchi uelewa wa masuala ya kiuchumi. Inatarajiwa kuwa itachochea uwekezaji na maendeleo katika Wilaya ya Tunduru.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.