Mkoa wa Ruvuma umebahatika kuwa na vivutio vya aina mbalimbali vya utalii likiwemo bwawa la Kaunde Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ambalo lina viboko wengi ambao wamekuwa kivuti kikubwa cha utalii.Wilaya ya Namtumbo imebarikiwa kuwa na vivutio vingine vya utalii ambavyo bado havija-wahi kuandikwa popote hivyo vikitangazwa na kufahamika vinaweza kuchangia maendeleo katika sekta ya utalii mkoani Ruvuma.
Katika kijiji cha Likuyusekamaganga kuna bwawa linaloitwa Kaunde lenye asili ya viboko wengi,pia Jumuiya ya Mbarang’andu imepandikiza samaki.Eneo hili linafikika kwa gari lipo kilometa tatu toka chuo cha maliasili Likuyu,katika bwawa hili unaweza kuweka kambi za muda(Temporary Camping.Katika kijiji cha Kitanda,eneo la Mbunde, kuna Shimo la Mungu(Gema la Mchatanila) hili ni gema refu ambalo kihistoria lilikuwa linatumika kuwatupa watu wakaidi dhidi ya viongozi wa jadi ambapo inaelezwa chini ya gema hilo kuna nguvu ya mvuta-no.Eneo lingine maarufu kwa utalii ni Msabala Mkuu katika kijiji cha Msindo,ambako kuna mli-ma mrefu wenye jiwe,inaelezwa Mmisionari alifika juu ya jiwe hilo na kupumzika na hatimaye msalaba ulikwekwa juu ya mlima huo kama kumbukumbu.Unaweza kufika katika eneo hili kupitia barabara ya Lumecha kwenda Hanga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.