Naibu Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema serikali inatarajia kujenga minara mitano katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma ili kuboresha Mawasiliano ya simu na intaneti hivyo kumaliza changamoto za mawasiliano kwenye Halmashauri hiyo.
Mhandisi Mahundi ametoa ahadi hiyo wakati anazungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa Kata za Wino,Matetereka,Mkongotema na Gumbiro katika Halmashauri ya Madaba akiwa katika ziara ya kikazi iliyolenga kusikiliza kero na changamoto za Mawasiliano ya simu,interneti na redio kutoka kwa wananchi ili kutafutia ufumbuzi wa kudumu na wananchi waweze kunufaika na Mawasiliano ya kidijitali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.