Changamoto ya mimba za utotoni zinavyofifisha ndoto za watoto wa kike Ruvuma
MKOA wa Ruvuma ulipokea taarifa ya matukio 811 ya mimba za utotoni katika kipindi cha mwaka 2020/2021.
Hayo yamesemwa na Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Ruvuma Mariam Juma wakati anasoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya jamii kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mwanaidi Ally Khamis.
Amesema kati ya matukio hayo,matukio 644 ni kwa kundi rika la umri wa miaka 16 hadi 17 na 167 ni kwa umri wa miaka kati kati 13 hadi 15.
Amekitaja chanzo cha taarifa hizo ni vituo vya kutolea huduma za afya 752,shule 46 jamii 19.
Hata hivyo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inaoongoza kwa kuwa na matukio ya mimba 343 sawa na asilimia 42,ikifuatiwa na Wilaya ya Namtumbo matukio 177 sawa na asilimia 21.8,Madaba matukio 109 sawa na asilimia 13.4 na Halmashauri ya Mbinga matukio 101 sawa na asilimia 12.5
“Matukio haya ya mimba za utotoni ,yanatishia usalama wa watoto wa kike,jitihada za kubadili tabia kwa jamii inahitajika ili iwajibike katika ulinzi na usalama wa watoto wa kike’’,alisema Juma.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mheshimiwa Mwanaidi Ally Khamis amesema amesikitishwa na matukio ya mimba za utotoni kwa sababu zinaathiri watoto wa kike kukatisha masomo hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao.
Amewashauri viongozi wa dini,wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuwalea watoto katika maadili mema.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.