• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

CHUO cha Taifa cha utalii chazindua mafunzo ya utalii kwa wadau

Imewekwa kuanzia tarehe: February 23rd, 2022

Chuo cha Taifa cha Utalii kimezindua mafunzo ya siku tano ya UVIKO 19 kwa wadau zaidi ya 140 waliopo kwenye mnyororo wa huduma za utalii katika Mkoa wa  Ruvuma ili kuwajengea uwezo wa namna ya kujikinga katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo wakati wanapotoa huduma kwa wageni  pindi wanapotembelea maeneo yao.

Akizungumza  wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika Februari 21,2022 Katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Mji wa Songea Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka amesema kuwa Mafunzo hao yamefadhiliwa na MPANGO WA TAIFA WA MAENDELEO KWA USTAWI WA TAIFA NA MAKABILIANO DHIDI YA UVIKO 19 kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii.

Dkt. Sedoyeka  amesema kuwa Chuo kimeamua kutoa mafunzo hayo kwa wadau wa utoaji wa huduma za Utalii baada ya kubaini kuwa baadhi yao walikuwa bado hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na Uviko 19 pindi wanapowahudumia watalii .

Amesema kuwa Chuo kinatoa mafunzo hayo kwa wadau muhimu katika mnyororo wa utalii ili wadau hao waweze kuboresha huduma zao na thamani ya pesa inayotolewa na mgeni au mtalii kuonekana. chuo kinatoa mafunzo hayo kwa watoa huduma hao kwa kuwa wengi wao hawana weledi wa utoaji huduma hasa wakati huu wa janga la UVIKO-19 ili kujikinga wao wenyewe pamoja na wageni wanaopata huduma zao.
Aidha, Dkt. Sedoyeka amesema mafunzo haya kwa mkoa wa Ruvuma yamekuja wakati sahihi ambapo kuna shughuli mbalimbali za utalii wa makumbusho, kupanda milima, fukwe n.k lakini watoa huduma kutokuwa na uelewa mpana na wa kibunifu wa kutoa huduma hizo.
Pia amesema  mafunzo yanatolewa katika mikoa nane ikijumuisha Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Mara na Mwanza. mbapo mpaka sasa mafunzo yamekamilika mkoa wa Lindi na Mtwara; yanaendelea mkoa wa Ruvuma na Njombe kwa siku tano,na badae kufikia mikoa mingine minne.
                                             Katika hatua nyingine Dkt. Sedoyeka  amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zinawezesha kukabiliana na Uviko 19 kwenye jamii pamoja na kwamba mpango huo unanesha nia madhubiti ya Serikali ya awamu ya sita Katika kukabiliana na janga hilo.

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa huo Brigedia Wilbert  Ibuge kwenye uzinduzi huo katika nafasi ya mgeni rasmi amesema kuwa sekta ya utalii imekuwa ikitoa fursa mbalimbali ikiwemo suala la ajira hivyo inatakiwa kuizingatia kikamilifu .

Ndaki amesema kuwa katika kipindi cha janga kubwa la Corona utalii uliyumba katika Nchi mbalimbali hivyo kwa sasa inatakiwa kuitumia elimu ya Uviko 19 ipasavyo ili kulinda watalii na jamii kwa ujumla .

Naye Maajabu Mbogo Afisa Utalii katika pori la Limbaramba ambaye ni mmojawa washiriki wa mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo hayo yataleta neema ya kuongezeka kwa watalii na kuifanya Serikali iweze kupata mapato kupitia watalii hao.

Hata hivyo Mbogo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka fedha za Uviko19 katika Sekta hiyo na kwamba RAIS ameangalia maslahi mapana ya nchi hasa katika kuikomboa Sekta ya Utalii nchini ambao imeathirika na Jana hilo kwa kiasi kikubwa.

Katika mafunzo hayo jumla ya mada Sita zitatolewa na wakufunzi wakufunzi mbalimbali kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii na mafunzo hayo yatafikia kilele chake ijumaa Februari 25,2022.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.