Meneja wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Songea, Dkt. Bakari Mashaka, amesema wanatarajia kuanza mradi mkubwa wa ujenzi wa chuo kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 10,000 wa kozi mbalimbali katika kata ya shule ya Tanga Manispaa ya Songea.
Amesema kwa sasa, IAA Kampasi ya Songea inatoa huduma zake kwenye jengo la TTCL, ghorofa ya pili, mjini Songea, na Kozi zinazotolewa ni diploma ya Usimamizi wa Biashara, Uhasibu na TEHAMA, Fedha na Benki, pamoja na masomo ya ngazi ya uzamili (Masters) katika fani za Biashara, Fedha, TEHAMA, Uongozi, na Usimamizi wa Rasilimali.
Dkt. Mashaka amesema kuwa chuo hicho kinalenga kuhakikisha wanafunzi wanajifunza kwa vitendo, hasa namna ya kuanzisha na kuendesha biashara ambapo ameeleza kuwa wanataka wanafunzi wao wasitegemee ajira pekee, bali wawe na uwezo wa kujiajiri na kuendesha maisha yao.
Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa IAA Kampasi ya Songea, Nuru Meshack, ameelezea changamoto kubwa waliyoibaini katika Wilaya ya Songea ni wazazi wengi kuamini kuwa mtoto aliyepata daraja la nne hawezi kuendelea na masomo, hivyo amewahimiza wazazi na wanafunzi kuwa ufaulu wa D nne, isipokuwa kwa masomo ya dini, unaruhusu mwanafunzi kujiunga na chuo.
Amewakaribisha wanafunzi kujiunga na IAA Kampasi ya Songea, akisisitiza kuwa chuo hicho kimejikita katika kuwasaidia wanafunzi kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na mazingira ya kusomea ni mazuri na yanasaidia mwanafunzi kufanikisha malengo ya kielimu na kuendana na teknolojia.
Chuo cha Uhasibu Arusha Kampasi ya Songea kinapatikana katika jengo la TTCL, ghorofa ya pili, karibu na ofisi za Manispaa ya Songea. Kwa mawasiliano zaidi namba 0784-171-565 au kufika moja kwa moja kwenye ofisi zao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.