Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba, ametembelea na kukagua, Mradi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA, Wilaya ya Nyasa ambao uko hatua za Mwisho za ukamilishaji.
Mh. Chilumba amekagua mradi huu, akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Nyasa.
Akizungumza mara baada ya kukagua Mradi huu, Mh Chilumba ameridhishwa na maendeleo ya ukamilishaji wa Mradi huu, na kusema kuwa anamshukuru Mh. Rais kwa Mradi wa VETA Nyasa,na Viongozi wote na Wananchi kwa ujumla wa Wilaya ya Nyasa kwa Ushirikiano wao wa kutekeleza Mradi mkubwa wa VETA.
“ Binafsi Nichukue Fursa hii kumshukuru Mungu kwa kufikia hapa, pia nimshukuru aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt John Pombe Magufuli kwa kutuletea Mradi huu, ambao ni mkubwa na unalengo la kutatua tatizo la Ajira kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa.Pia nashukuru Mh.Rais Samia Suluhu Hasan na ninamhakikishia kuwa Wilaya ya Nyasa ina uwezo wa kutekeleza Miradi mikubwa ya Maendeleo”.
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Nyasa na Wilaya jirani, kutumia fursa ya Chuo cha Ufundi stadi cha Nyasa pindi kitakapoanza kutoa mafunzo ya Ufundi.
Kukamilika kwa Mradi wa chuo cha Ufundi Stadi Nyasa, Serikali imetatua changamoto ya Chuo cha Ufundi Stadi Wilayani hapa kwa kuwa awali hapakuwepo na chuo hiki na Iliwalazimu wananchi kutembea umbali wa Kilometa 165 kufuata vyuo vya Ufundi stadi Wilaya ya Songea.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.